MAPOKEZI YA MGIMWA JIMBO LA KALENGA YATIA FORA KILA ANAKOPITA
Kila mtu anahamu ya kumsalimu |
Wengine anashindwa kujizuia na kuamua kuzungumza nao |
Wengi wanamtakia kila la kheri |
Akwilombe akimuombea kura katika mikutano iliyofanyika katika vijiji sita hii leo |
MGOMBEA
ubunge wa Uchaguzi Mdogo Jimbo la Kalenga kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)
Godfrey Mgimwa jana aliiteka kata ya wasa katika kampeni za za kuomba uwakilishi
wa jimbo hilo.
Katika
kila kijiji alichopita katika kata hiyo, Mgimwa alilazimika kutumia dakika 10
hadi 20 kusalimiana na wapiga kura wake kwa kushikana nao mikono.
Katika
mikutano yake tofauti kwenye vijiji vya Usengelendete, Mahanzi, Ihomasa,
Ikungwe, Wasa na Ufyambe, hotuba ya
Mgimwa ilikuwa ikikatizwa mara kwa mara na makofi ya wananchi waliokuwa
wakimsikiliza.
“Nawapenda
kama navyoipenda familia yangu; nawahakikishieni kwa kupitia mbinu mbalimbali
za utekelezaji wa Ilani ya CCM nitahakikisha ahadi zote zilizotolewa wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa 2010 zinatekelezwa,” alisema.
Aliwataka
wananchi wa kata hiyo na jimbo hilo kwa ujumla kumsaidia ili atumie maarifa
aliyonayo kuwasaidia.
“Msinipime
kwa umbo langu dogo, nipimeni kwa utekelezaji wa ahadi ninazotoa;
nawahakikishieni mtoto wa nyoka ni nyoka, ahadi zote zilizotolewa na marehemu
baba yangu nitahakikisha zinatekelezwa,” alisema.
Alisema
ana elimu nzuri sana ambayo hataki kuitumia kwa kazi nyingine yoyote ila kwa
kushirikiana na wananchi wa jimbo hilo kuharakisha maendeleo.
Alisema
anafahamu changamoto zinazoikabili sekta ya kilimo, maji, elimu, afya, barabara
na umeme katika jimbo hilo na akaahidi baada ya kuapishwa atawabana baadhi ya
viongozi ili wamsaidie kuzitekeleza.
“Mtu
wa kwanza atakuwa Waziri Mkuu akiwa kama msimamizi wa shughuli za serikali
bungeni; lakini na mawaziri wa sekta nyingine zinazohitaji ufanisi katika jimbo
hili,” alisema.
Mmoja
wa wapiga debe wa mgombea huyo, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe
alisema “huu ni uchaguzi mdogo, sio uchaguzi ambao kila chama kinachoshiriki
kinatafuta ridhaa ya wananchi ili kiunde serikali.”
Alisema
litakuwa jambo la kushangaza kama wananchi wa jimbo hilo watampa kura mgombea
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ili akawa mwakilishi wao.
Akitoa
mfano alisema haiwezekani mtu mwenye suruali nyeusi iliyotoboka akaweka kilaka
cha kitambaa chenye rangi nyeupe.
“Aliyekuwa
mbunge wa jimbo hili ni mwana CCM, sasa tunawezaje kuziba pengo lake kwa kuweka
mbunge kutoka chama kingine,” alisema katika mikutano hiyo.
Alisema
Chadema wanajua kwamba katika uchaguzi huo wameingia wakiwa wanaenda kushindwa
na sasa wanazo kazi mbili wanazoendelea kufanya jimboni humo.
Alizitaja
kazi hizo kuwa ni pamoja na kutumia wafuasi wao kutoa Arusha na Kilimanjaro
kuwashawishi kwa fedha baadhi ya wana CCM ili wawauzie shahada zao za kupigia
kura.
“Lakini
pili wanatengeza mazingira ya fujo, ili kuwaogopesha wazee, kinamama, kinababa
na vijana ili wasijitokeza kwa wingi kumchagua mgombea wao wanayemtaka,”
alisema.
Aliwaomba
wananchi kushirikiana na viongozi wa CCM katika maeneo yao kwa kutoa taarifa za
watu hao ili wakamatwe na kufikishwa kwenye vyombo vya dola.