Siku za kwenda Brazil Kombe la Dunia ziko ukingoni
Ni
siku 100 tu, ni vigumu kuamini kuwa iko karibu. Inaonekana kama jana tu
kwamba Brazil imethibitishwa kuwa muandaaji wa FIFA World Cup 2014.
Nakumbuka msisimko niliohisi na kuona kuwa nchi yangu inaenda kwenye
hatua muhimu ya mpira katika Dunia hii.
Hata ingawa mimi sitakuwa uwanjani, lakini nimeanza kupata vipepeo
tumboni kama ambavyo nilikuwa nikikaribia mechi kubwa. Baada ya yote
kumalizika FIFA World Cup, itakuwa ni ya aina ya mwisho kwa Brazil,
tofauti na kujitangaza yenyewe kimataifa. Uangalizi utakuwa juu yetu na
ni nafasi kubwa kwetu kwa kuionyesha Dunia umuhimu kuhusu Brazil na watu
wa Kibrazil walivyo.
Wakati wa Kombe la Dunia la Olimpiki 2016 itakayofanyika Brazil,
tutakuwa na nafasi ya kuionyesha Dunia jinsi tunavyo penda michezo na
vilevile tulivyo na nguvu katika uchumi wetu. Brazil ni kiongozi mkubwa
Duniani kiteknolojia na kiongozi mkubwa wa uzalishaji wa Nyama, madini
na mzalishaji mkubwa wa soya duniani. Ni karibu sasa maelfu ya watalii
na waandishi wa kigeni watafika kwenye mlango wetu ulio wazi kujionea na
kugundua uhalisia wa Wabrazili.
Ingawa Brazili ni nchi kubwa kijamii, lakini tumefanya mambo mengi
ya kukabiliana na matatizo katika miaka ya hivi karibuni.
Tuna
utaifa tofauti lakini tuna umoja mzuri kijamii na kimaendeleo katika
ubunifu wa juu. Ni nchi iliyojaliwa watu wenye uwezo mkubwa kiakili na
inawatu wengi wenye vipaji vikubwa katika michezo kama Neymar
anavyocheza na maajabu yake ya kuchezea mpira . Vilevile mziki wa Tom
Jobim na sayansi aliyoipata kutoka kwa Miguel Nicolelis, kama utafiti
waliofanya na kupata matumaini kuwa siku moja mifupa ya binadamu inaweza
kutembea tena.
Brazili ni nchi nzuri sana, na ni nchi iliyobarikiwa kuwa na hali ya
asili nzuri. Watalii wote watakaofika Brazil wakati wa Kombe la Dunia
wajiandae kukutana na hali ambayo hawataisahau na hawajawahi kuiona.
Vilevile watafurahia kutembelea fukwe za kusini na kujionea misitu na
mto wa Amazon, milima katika mji wa Rio de Janeiro ambayo ni sehemu
muhimu sana kwa watalii. Naamini kila mtalii ataondoka Brazil akiwa na
kumbukumbu nzuri katika maisha yake yote.