Uvutaji sigara unawaathiri watoto
Utafiti mpya kutoka ulaya na
marekani kazkazini unasema kuwa,kupigwa marufuku kwa uvutaji wa sigara
hadharani kumesababisha kushuka kwa viwango vya wanawake kujifungua
mapema kabla ya mda wao kwa asilimia 10.
Idadi ya watoto waliolazwa hospitalini kutokana
na ugonjwa wa pumu pia imepungua kwa asilimia 10% katika maeneo ambayo
uvutaji sigara hadharani umepigwa marufuku kulingana na wanasayansi
kutoka chuo cha Edinburgh nchini Scotland.Mmoja ya waanzilishi wa utafiti huo Prof Aziz Sheikh ambaye ripoti ya utafiti wake imechapishwa katika jarida la matibabu duniani Lancet,anasema kuwa mataifa yasio na marufuku hiyo yanapaswa kutilia maanani matokeo hayo kwaajili ya kizazi chao cha baadaye.
Kwa sasa ,sheria dhidi ya uvutaji sigara zinaathiri asilimia 16 ya idadi ya watu dunaini.