CHELSEA YAREJEA KILELENI ENGLAND
KLABU ya
Chelsea imerejea rasmi kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England,
kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stoke City Uwanja wa Stamford
Bridge usiku huu.
Mohamed Salah akicheza mechi yake ya kwanza The Blues, alifunga bao la kwanza dakika ya 32 pasi ya Nemanja Matic, kabla ya mkongwe Frank Lampard kufunga la pili dakika ya 61 na Willian kukamilisha ushindi dakika ya 72 kwa bao la pasi ya Salah.

Kikosi
cha Jose Mourinho kilijikuta katika wakati mgumu baada ya kufungwa na
Crystal Palace wiki iliyopita, lakini sasa matumaini yamerejea baada ya
kufikisha pointi 72 kutoka michezo 33.
Liverpool yenye pointi 71 za mechi 32, ambayo inacheza na West Ham kesho na Manchester City iliyoifunga 4-1 Southampton mapema leo na kufikisha
Liverpool yenye pointi 71 za mechi 32, ambayo inacheza na West Ham kesho na Manchester City iliyoifunga 4-1 Southampton mapema leo na kufikisha
pointi 70
za mechi 31, ndio washindani wakuu wa Chelsea katika mbio za ubingwa
msimu huu. Aidha, ushindi huo unamfanya Mourinho afikishe mechi 77 za
kucheza nyumbani bila kufungwa.(P.T)