HARAFU BADO MNASEMA DIAMOND ANAPESA KAZI IPO KWA MSANII RAY ASEMA UTAJIRI WAKE HAKUNA MSANII YEYOTE ANAEMFIKIA
Ray
Star wa filamu nchini Vicent Kigosi "Ray" amesema kuwa yeye ana pesa
na mali nyingi na hakuna msanii yeyote wa Tanzania awe wa filamu au
muziki anayemfikia sema hapendi tu kujitangaza kama baadhi ya mastaa
wenzake akidai ni ulimbukeni. "hakuna msanii anayenizidi uwezo kuanzia
mali na hata fedha niko mbali sana mimi, hata gari ninalotembelea hakuna
msanii aliyenalo kama ingekuwa ni mtu wa kujisifusifu na kutafuta sifa
za kijinga jamii ingejua" alisema star huyo wa filamu za Oprah, Sobbing
Sound, Hard Price na Handsome Wa Kijiji akizungumza na gazeti moja.
Ray vile vile aliamua kurusha kombora kwa wabaya wake wasiopenda
maendeleo yake kwa kusema "wanaongea sana majungu, fitina na vitu
ambavyo havipo kuhusu mimi, mimi ni jembe, kwanini wasiangalie maisha
yao? leo msanii unateta nae dakika hiyo hiyo anageuza maneno hayo kuwa
majungu, acha nikae peke yangu nifanye issue zangu"