UNDANI VIFO VYA WATOTO 3 NDANI YA BWAWA INASIKITISHA!
KUFUATIA vifo vya watoto watatu waliokufa kwa pamoja ndani ya bwawa la kuogelea ‘swimming pool’ kwenye Hoteli ya Landmark, Mbezi Beach jijini Dar, undani wa vifo hivyo umejulikana, Amani lina kisa kamili.
CHANZO
Kwa
mujibu wa chanzo chetu, watoto walionusurika kufa ambao walikuwa
wakisherehekea siku ya kuzaliwa ya mwenzao ‘bethidei’ aliyejulikana kwa
jina la Derrick Mboka, waliwaona marehemu wakielea kwenye maji ya bwawa
hilo walilosema kuwa ni la kuogelea watu wazima.
UZEMBE WATAJWA
Habari
zaidi zinadai kuwa sababu kubwa iliyosababisha vifo vya watoto wote
watatu ni uzembe uliofanywa na walinzi wa bwawa hilo ambao walidaiwa
kutokuwa makini kuwadhibiti watoto wengi waliokuwa wakiogelea karibu na
bwawa la watu wazima kiasi cha kutoka na kuingia huko.
MAMA WA MTOTO MWENYE BETHIDEI ATUPIWA LAWAMA
Uzembe
mwingine ulitajwa kufanywa na mama wa mtoto aliyekuwa akisherehekea
siku yake ya kuzaliwa aliyetajwa kwa jina la Anita Mboka kwa kuwachukua
watoto wasio wake na kuondoka nao bila kutoa taarifa kwa wazazi wao japo
kuwa mama wa marehemu Janeth Zakaria (9), Devotha Mbutwa alikiri
kupokea taarifa kuwa mwanaye anakwenda kwenye bethidei ya mwenzake beach
(baharini).
TAARIFA ZA MTOTO WA PILI
Kwa upande wao, ndugu wa karibu wa marehemu Ndimbumi Bahati (9) walisema hawakupata taarifa yoyote kuhusiana na mzazi huyo kumchukua mtoto huyo, wakadai siku ya tukio, marehemu alipelekwa na baba yake kula chipsi jirani na alipomaliza, baba aliondoka akimuahidi kuwa atakaporejea angemchukua kumpeleka matembezini, lakini jioni akapata taarifa amefariki dunia.
Marehemu alizikwa jana jijini Mbeya.
KUHUSU MTOTO WA TATU
Nao ndugu wa mtoto marehemu Eva Nicholaus (11) hawakupatikana mara moja kwa kuwa hadi gazeti hili linaelekea mtamboni hakukuwa na msemaji rasmi wa familia hiyo ambayo msiba wake ulikuwa Kijitonyama-Mpakani, Dar. Alizikwa jana Makaburi ya Sinza jijini Dar.

WAZAZI WAVIPOKEA VIFO KWA MTAZAMO TOFAUTI
Inadaiwa baada ya vifo vya watoto hao wa mtaa mmoja, kuna wazazi walivipokea vifo hivyo kwa mtazamo tofauti ambapo kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa familia ya Ndimbumi, baba wa mtoto huyo, Bahati Sisala alikuwa amechanganyikiwa kiasi cha kupoteza fahamu kwa siku nzima.

KIJITONYAMA YAZIZIMA
Waandishi wetu walishuhudia wakazi wa Kijitonyama mahali walipokuwa wakiishi watoto hao wakiwa katika majonzi makubwa ambapo umati uligawanyika kuaga watoto hao.

WANAFUNZI WAMLILIA MWENZAO MSIBANI
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kijitonyama ambao walikuwa wakisoma na Ndimbumi walifika katika msiba huo na kusikitisha waombolezaji waliohudhuria msibani hapo baada ya kuangua vilio jambo lililoongeza simanzi. Marehemu alikuwa akisoma darasa la nne.
MWENYEKITI, AFISA ELIMU NA KIONGOZI WA DINI WANENA
Kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Mtaa wa Kijitonyama, Alhaus Magoha alisema amesikitishwa sana na vifo hivyo vilivyotokea ndani ya mtaa wake na kuongeza kuwa hilo ni pigo kubwa.

HOTELI YAGHARAMIA USAFIRI
Habari zilizopatikana wakati gazeti hili linakwenda mitamboni zilisema kuwa, uongozi wa Hoteli ya Landmark ndiyo uliojitolea kubeba jukumu la kuisafirisha miili ya Ndimbumi na Janet.
Juzi waandishi wetu walifika kwenye hoteli hiyo kwa lengo ka kuzungumza na uongozi lakini waliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa kwenye vikao.