HAKIKA INASIKITISHA UNYAMA WA BINADAMU ULIOKITHIRI HUU HAPA
Mtoto Nasra akiwa katika wodi ya watoto hospitali ya mkoa wa Morogoro anakopatiwa matibabu kwa sasa.
Baba
mzazi wa mtoto huyo alisema yeye ana mke na watato wengine wa ndoa na
kwamba hakuwahi kumwambia mkewe kama ana mtoto wa nje hivyo ilikuwa
vigumu kumchukua mtoto huyo na ndipo alipomkabidhi mama mkubwa wa mtoto huyo.
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto huyo kutoka ndani ya nyumba ya mama yake
huyo mkubwa, ghafla kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe,
walianza kumshambulia mwanamke huyo, kitendo kilichomlazimisha
(mtendaji) kutoa taarifa polisi.
Alisema mtoto huyo anamaumivu makali sehemu ya mgongo na mikono na kwamba mwili wake pia ni mteke kama wa mtoto mchanga hali inayowafanya kuendela kumfanyia uchunguzi wa kina zaidi.