KINANA, NAPE WATINGA NYUMBANI KWA LIPUMBA TABORA, WASHUHUDIA BENDERA CUF ILIYOCHANIKA IKIWA KWENYE NYUMBA YAO KATIKA KIJIJI CHA ILILONGULU
Bendera ya Chama cha Wananchi (CUF), kinachongozwa na Mwenyekiti,
Profesa Ibrahim Lipumba ikipepea huku ikiwa imechanika nyumbani kwao
katika Kijiji cha Ilolangulu, Jimbo la Kaskazini, Wilaya ya Uyui,
Tabora. Bendera hiyo ilinaswa leo mchana wakati Katibu Mkuu wa CCM,
Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye
walipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika
mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Ilolangulu, huku mbele yake
ikionekana nyumba iliyowekwa bendera ya CUF, iliyochanika kwenye nyumba
(inayoonekana) nyumbani kwa Mwenyekiti wa CUF, Ibrahim Lipumba katika
kijiji hicho.Nape alisema si vizuri kwa kiongozi mkubwa wa CUF, Profesa
Lipumba kuwepo na hali kama hiyo.
Sehemu ya umati wa watu ukisikiliza kwa makini katika mkutano huo wa CCM.
Askari wa Usalama barabarani wakipita karibu na nyumba hiyo.
Nyumbani kwa akina Profesa Ibrahim Lipumba, katika Kijiji cha Ilolangulu ikipepea bendera ya CUF ikiwa imechanika.PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG