Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahtubia wakazi wa Loya wilayani Uyui,Katibu Mkuu aliipongeza sana halmashauri ya wilaya kwa kujenga shule za sekondari 18 za kata. Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Uyui Mussa Ntimizi akihutubia wakazi wa Loya wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika hapo ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameanza ziara katika wilaya ya Uyui ikiwa wilaya ya tatu baada ya kumaliza Nzega na Igunga. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Loya ambapo aliwapongeza sana kwa kuwa wa moja kwa kushikana na chama chao na kusema ukweli kwa changamoto zinazowakuta kisha kwa pamoja kupata ufumbuzi.(P.T) Mbunge wa jimbo la Igalula Ndugu Athumani Juma Mfutakamba akihutubia wananchi wa Loya ambapo aliwahakikishia kuwa mnara wa mawasiliano utawekwa kwenye kata hiyo ambayo mawasiliano ni tatizo kubwa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi ya aina yake kutoka kwa wamamchi wa Kata ya Kizengi wilayani Uyui. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi kufungua ofisi za CCM kata ya Kizengi wilayani Uyui. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia vitabu wakati alipotembelea shule ya sekondari ya kata ya Loya wilayani Uyui mkoani Tabora. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akifurahi baada ya mwanafunzi wa kidato cha tatu wa shule ya sekondari Lutende Ngasa Shigela kumwambia kuwa ana taka kuwa Mbunge miaka ijayo na kusisitiza kazi ni kusaidiana. Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Kizengi wilayani Uyui ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa viongozi wa kisiasa kama hawazungumzii masuala ya wananchi basi watakuwa hawatendi haki kwa wananchi wao. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Kata ya Kizengi ambao wamekuwa na kilio cha muda mrefu cha kuomba eneo zaidi la kuchungua mifugo kutokana na sehemu kubwa ya ardhi kuwa chini ya hifadhi ya Taifa. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM Lucia Stefano,zaidi ya wanachama 300 wamejiunga na CCM katika kata ya Kizengi.