Alysia Montano, mwanariadha wa kike na mshiriki wa Olympic aliyewahi kushinda mara tano mashindano ya riadha ya Marekani ambaye hivi sasa anaujauzito wa miezi 8, bado anashiriki riadha na hali aliyonayo. Alysia amewashangaza wengi baada ya kukimbia umbali wa mita 800 kwa dakika 2 na sekunde 32 huko California, juzi (June 26), ikiwa amechelewa sekunde 35 tu ya uwezo wake wakati akiwa hana ujauzito. Mwaka 2010, mwanamke huyo akiwa katika hali nzuri alikimbia mita 800 kwa dakika 1 na sekunde 57. Mwanariadha huyo ameeleza kuwa yeye anajisikia vizuri kukimbia umbali huo akiwa na ujauzito na kwamba amekuwa akifanya hivyo katika kipindi chote cha ujauzito na ameruhusiwa na daktari. “I've been running throughout my pregnancy and I felt really, really good during the whole process.” Alisema baada ya kumaliza kukimbia.