Askofu Alinikisa Cheyo wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi
Askofu
Alinikisa Cheyo wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi lililo
na Makao yake Makuu eneo la Jacaranda Jijini Mbeya amekanusha waraka
unaosambazwa ili kumshinikiza ajiuzuru nafasi ya Uaskofu.
Cheyo
amesema waraka unaodaiwa kusambazwa na Baraza la Wazee wa Ushirika wa
Bethelehem bado hajaupata ofisini kwake na kwamba kitendo hicho ni kukiuka
maadili ya utumishi wa Kanisa na Katiba ya Moravian Jimbo la Kusini Magharibi.
Waraka
huo uliosambazwa katika Shirika mbalimbali na Taasisi za Kanisa na kufanikiwa
kupata nakala yake ukiwa umesainiwa na Katibu wa Baraza R. Kalinga na
Mwenyekiti wa Baraza Mchungaji wa Ushirika wa Bethelehem Edward Chilale.
Askofu
Cheyo ambaye yuko kikazi Dodoma alisema kuwa kitendo kilichofanywa na Mchungaji
Chilale ni cha utovu wa nidhamu na anafanya hivyo kujihami kutokana na maamuzi
magumu na hatua ambazo zinatarajiwa kuchukuliwa na Halmashauri Kuu ya
Jimbo.
Hata
hivyo Wachungaji wengine walisema hawakubaliani na waraka uliotolewana Baraza
la Bathelehem na kwamba hizo ni chuki binafsi za Mchungaji Chilale baada ya
kuonywa kuacha biashara za Pentagon,Elimisha na Madawa ya GNLD ambapo amekuwa
akikusanya fedha kutoka kwa waumini na wasio waumini.
Wachungaji
hao ambao hawakupenda kutaja majina yao walisema pia Mtunza hazina wa Ushirika
huo ambaye pia ni Mtumishi wa Umma ndiye amekuwa akiufadhili mgogoro huo kwa
kutoa gari lake na kusambaza barua za uchochezi katika shirika mbalimbali.
Wameenda
mbali zaidi kwa kusema kuwa kama ni maamuzi ya Baraza la Bethelehem iweje
waraka huo usambazwe katika sharika nyingine wakati kila baraza lina maamuzi
yake hivyo ni kuingilia utaratibu na kuwanyima waumini na Taasisi uhuru wa
kujadili agenda zao.
Mgogoro huo umekuwa ukizidi kushika kasi
siku za hivi karibuni na kuzidi kuligawa Kanisa kimwili na kiroho kwani badala
ya kujadili maendeleo ya Kanisa, waumini na Viongozi wamekuwa wakipoteza muda
kujadili mgogoro bila kupata ufumbuzi wowote.
|