HAYA NI MAKUBWA ZAIDI YA MAKUBWA JAMANI:_ TAZAMA HAPA TUKIO LA AINA YAKE SHINYANGA,MADIWANI WA CHADEMA WALIOHAMIA CCM,WARUDI CHADEMA TENA
Waliletwa na pikipiki kwenye mkutano_Aliyevaa nguo ya kijani(CCM) ni bwana Zacharia Mfuko diwani wa CHADEMA kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga baada ya kuwasili katika mkutano wa Chadema leo jioni,baadaye alivua nguo hizo na kuomba radhi kuwa alikosea njia baada ya kushawishiwa na viongozi wa CCM akiwemo Stephen Masele,Nape Nauye, Habib Machange na viongozi wengine wengi ndani na nje ya chadema na CCM,na kueleza kuwa ccm hawana lolote badala ya kulaghai watu kwa kutumia pesa. |
Madiwani wasaliti kama wanavyoitwa hivi sasa hapa Shinyanga,wakiwa na nguo za CCM wakiwa wamekaa na viongozi wa CHADEMA baada ya kuwasili eneo la mkutano jioni ya leo.
Mkutano huo ni wa aina yake umehudhuriwa na maelfu ya wananchi wa mkoa wa Shinyanga,kila mtu akiwa na lake moyoni,wengine wakisema CHADEMA wawapige chini madiwani hao,wengine wakisema wasamehewe kwani mungu karudisha kondoo wake waliopotea.
Diwani Sebastian Peter kulia akinong'ona jambo na mbunge Kasulumbayi. |
Wengine walilia kwa hasira_Wananchi wakiwa hawaamini kilichokuwa kinaendelea uwanjani hapo,matusi yalitawala. |
Ilikuwa siyo hali ya kawaida-wengi walibaki midomo wazi,walipigwa na hali ya mshangao,wenye kushika viuno haya,wenye kununa haya,wenye kutukana haya,wenye kusema bora liende nao walikuwepo,wenye kuisikitikia chadema kwa kupokea watu wanafiki na wasaliti haya,wenye kukumbuka mbwembwe za CCM wakati wa kuwanyakua madiwani hao wa chadema tena katika eneo hill hilo nao hawakukosekana. |
Madiwani hao wawili wakiwa jukwaani tayari kuzungumza na wananchi wa Shinyanga,kulia ni mbunge Kasulumbayi akiwakaribisha.Picha na Kadama Malunde-Malunde1 blog |
Tunavua uccm-Kama walivyovua magwanda ya CHADEMA mbele ya Nape Nauye wa CCM,leo madiwani hao wamevua pia nguo za CCM,lakini tofauti na kipndi kile leo hawakuchoma moto nguo. |
Mbunge Kasulumbayi akiwa ameshikiria nguo za CCM za Sebastian Peter na Zacharia Mfuko,akasema CHADEMA haina chuki na ccm hivyo kusisitiza kuwa kamwe hawawezi kuchoma moto nguo hizo ila yeyote anayezipenda basi akachukue. |
Kushoto ni Zacharia Mfuko baada ya kuvua nguo za CCM,akiwaomba msamaha wanachama wa chadema na wananchi kwa ujumla.Alisema walihadaiwa na CCM,kamwe hatarudia kosa na kuongeza kuwa hata nguvu za giza/dawa/uchawi zilitumika kuwachanganya akili ili waidharau chadema lakini sasa wamegundua ujanja wa ccm na kuwatahadhalisha wengine wenye nia ya kwenda CCM waache kwani hakifai. |
Kushoto ni Sebastian Peter baada ya kuvua nguo za CCM,akizungumza jukwaani ambapo aliwataja viongozi wa ccm walioshiriki katika mchakato mzima wa kuwahadaa kuwa ni mbunge wa Shinyanga mjini Steven Masele,Ridhiwani Kikwete,Habibu Machange,Mwigulu Nchemba,(Emmanuel Kidenya,Zenna Musa Gulam na mwingine aliyejulikana kwa jina la moja Eliza- hawa ni makada wa Chadema).Leo wamerusha kombora kwa mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi kwa kushirikiana na viongozi wengine wa ccm kuwa walikuwa wameahidi kuwapa shilingi milioni 50 madiwani hao ili wasiende kwenye mkutano wa leo. |
......Hiki ninachokiona sasa hivi ni ndoto,mazingaombwe au ndiyo kile waungwana wanachosema kuwa siasa ni mchezo mchafu |
Katikati ni diwani wa viti maalum kata ya Masekelo(anayotoka Zacharia Mfuko) bi Zainabu Kheri akitafakari jambo kwenye eneo la mkutano |
Baada ya kutangaza kurudi tena chadema na kukaribishwa tena kwa mikono miwili madiwani hao wakiwa wamekaa na viongozi wa chadema,kabla ya kutoroshwa kimya kimya eneo la mkutano wakati mkutano ukiendelea....Hofu ni usalama wa maisha ya madiwani hao. |
Wananchi wakishangaa namna madiwani hao walivyotoroshwa uwanjani hapo na gari ambayo haikujulikana ilitokea wapi. |
Hiyo ndiyo gari iliyotumika kuwatorosha madiwani waliohamia tena Chadema baada ya kudai kushindwa majukumu waliyopewa na viongozi wa ccm ikiwemo kutekeleza mauaji ya baadhi viongozi wa CHADEMA akiwemo Dr Slaa .Ikumbukwe pia kuwa wakati wanahamia ccm madiwani hao waliwatuhumu viongozi wa juu wa chadema kuwa walitaka kumuua mbunge wa shinyanga mjini wa ccm Steven Masele. |
Mbunge Kasulumbayi akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwakaribisha madiwani hao na kwamba sasa ni madiwani tena kwa sababu wakati wanajiuzulu hawakufuata taratibu kama vile kwenda mahakamani,kuwasilisha vitambulisho vya udiwani na vyeti vyao vya ushindi na kuwashangaa CCM kwani hawako makini kwa sababu hawakujua kuwa watu waliowachukua ni wajanja kwa vile hata kadi za ccm hawakuchukua na wamefanikiwa kujua siri za ccm na mipango yao katika kuimaliza CHADEMA na kamwe hawataweza. |
Katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga ,ambaye pia ni mwenyekiti wa wazee chadema taifa Nyangaki Shilungushela maarufu kama mzee wa utaratibu akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kilichotokea leo ni mchezo wa siasa kwani katika siasa hakuna uadui wala urafiki leo yanatokea haya kesho mengine ni utaratibu tu. |
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga bi Siri Yasin akifunga mkutano leo jioni. |