Makubwa haya!!! MCHUNGAJI MTIKILA AMFUNGULIA KESI ASKOFU MOKIWA KWA KOSA LA KUMPAPASA MAKALIO YAKE
Mchungaji Christopher Mtikila.
Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kumshitaki Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglican Tanzania Dk. Valentino Mokiwa.
Msingi
wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika makalio Mtikila na kwamba
kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana walipokutana maeneo ya
Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila
alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko la Mtikila kwamba Kanisa la
Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo wizi wa vifaa vya Hospitali
ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa mkoani Njombe.
Mtikila
alivyoitwa na Askofu Mokiwa ili kujadili hilo alifika na wenzake watatu
wa taasisi ya Liberty International Foundation na wakakaribishwa kwenye
moja ya jengo la dayosisi ya St. Nicholous, usiku wa saa 03:00.
Muda
mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa ambaye alikuwa na wenzake
saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe kama kuna mtu ana
kinasa sauti. Baadae Askofu Mokiwa nae alisimama na kuungana na wenzie
kuwakagua kina Mtikila baada ya kuhakikisha mlango umefungwa.
Katika
upekuzi huo ndipo tuhuma hizo zilipopatikana kutokana na madai kwamba
operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya lengo la kawaida.
Wakili wa Upande wa mashtska aliiambia mahakama kuwa,“Mlalamikiwa
alitangaza kuwa, kila mtu aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe
na kwamba atakayekataa angetumia nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola,
hakuna aliyebisha.”
Alisema kisha akaendelea “Mshtakiwa
(Mokiwa) alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo kuelekea chini
kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi ikipapasa
makalio ya mlalamikaji”.
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha.
Madhara
zaidi ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi,
aibu katika jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na
matatizo ya moyo kila anapokumbuka kitendo hicho.
Kesi inasikilizwa kwenye Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, chini ya Hakimu Agness Mchome