RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM
KATIBU MKUU KIONGOZI AKUTANA NA UJUMBE TOKA CHUO CHA ST THOMAS CHA MAREKANI
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM jijini Dar es salaam leo.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiongea na ujumbe kutoka
Chuo cha St. Thomas cha Marekani uliomtembelea Ikulu jijini Dar es
salaam leo Julai 16, 2014 Picha na Ikulu
Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Y. Sefue leo tarehe 16 Julai, 2014 amekutana na wanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Mt. Thomas cha Minnesota, Marekani wanaotembelea
Tanzania kujifunza uzoefu wa Tanzania katika masuala ya kiuongozi na
anuwai ya tamaduni. Wanafunzi hao ambao kwa idadi yao ni wanafunzi 14
wanaochukua Shahada za Uzamivu na Uzamivu katika masuala ya Uongozi wa
Kimataifa pamoja na Wakufunzi wao wawili, Dkt. Jean Pierre Bongila na
Dkt. Artika Tyner.
Mkutano
huu ni mwendelezo wa mkutano kama huu ambao Katibu Mkuu Kiongozi
aliufanya mwaka jana na kundi jingine la wanafunzi kutoka Chuo hicho
ambapo aliwapa uzoefu wa uongozi na anuwai ya tamaduni katika Tanzania,
Afrika na katika medani za kimataifa.
Kwa
kutambua umuhimu wa nasaha walizozipata wanafunzi wa mwaka jana, Chuo
hicho kiliomba na kukubaliwa fursa nyingine ya kuonana na Katibu Mkuu
Kiongozi. Ziara ya wanafunzi hao ilianzia Arusha tangu tarehe 12 Julai,
2014 na itamalizika tarehe 17 Julai, 2014.
Pamoja na
kupata fursa ya kuonana na kuzungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa
Arusha, wanafunzi hao walipata pia muda wa kutembelea vivutio mbalimbali
vya utalii vilivyopo Arusha na baadaye Zanzibar. Na matarajio ni kuwa
wanafunzi hao watakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania sehemu
mbalimbali za dunia watakakokwenda kufanya kazi.
Kwa
ujumla, wanafunzi wamepata fursa nzuri ya kuuliza maswali yaliyogusa
maeneo yote yanayohusu uongozi, siasa, uchumi, elimu, afya na utamaduni
ambayo yalipata ufafanuzi wa kutosha kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.