Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (katikati), akiongozwa polisi
kuingia kwenye gari baada ya kutokea vurugu meza kuu, katika mkutano wa
hadhara uliofanyika Kata ya Goba, Kinondoni Dar es Salaam, ambazo alidai
zilipangwa kwa makusudi na viongozi wa Chadema kwa lengo la kumvulugia
ziara yake ya kuwaelezea wananchi utekelezaji wa Ilani ya CCM katika
suala la upatikanaji wa maji ya uhakika jijini Dar es Salaam ifikapo
Septemba, mwakani. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Gari lililombeba Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, likilindwa na
polisi lililopokuwa linaondoka baada mkutano wa hadhara kuvunjika
kulikosababishwa na vurugu ambazo waziri alidai kuwa zilipangwa kwa
makusudi na wafuasi pamoja na viongozi wa Chadema waliokuwa wakirumbana
na viongozi wa CCM, katika Kata ya Goba, Kinondoni, Dar es Salaam.
Makalla alikuwa katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika mikoa ya
Dar es Salaam na Pwani.
Makalla akijadiliana na maofisa wa CCM na Polisi kabla ya kwenda kupanda gari na kuondoka.
Poilisi wakiwadhibiti baadhi ya wafuasi wa Chadema waliokuwa
wakisababisha vurugu katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya
Makongo. Kinondoni.
Polisi wakimdhibiti mmoja wa viongozi wa Chadema wakati wa mzozo
uliotokea jukwaa kuu katika mkutano wa Naibu Waziri wa Maji, Makalla na
wananchi wa Kata ya Goba.
Kiongozi wa cHADEMA AKIZOZANA NA WA ccm jukwaani katika mkutano wa Makongo Juu.
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee akizoza jukwaani katika mkutano uliofanyika katika Kata ya Goba na hatimaye kuvunjika
Polisi wakimdhibiti mfuasi wa Chadema asiendelee kufanya fujo katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kata ya Goba
Askari wa FFU, akilinda doria wakati waziri Makalla akikagua nyumba
ambazo watu wamejiunganishia isivyo halali eneo la Bonde la Msimbazi,
Dar es Salaam.
Makalla na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (kushoto) wakiangalia pampu
zinazotumika kujazia maji kwenye malori yanayonyonywa kutoka kwenye
mabomba ya Dawasa. Pampu hizo zilinaswa uani mwa nyumba katika eneo la
Bonde la Mto Msimbazi Dar es Salam
Waziri Makalla na viongozi wengini wakishanga kuona tanki kubwa la maji
lililojengwa chini ya moja kati ya nyumba tano katika eneo hilo ambazo
wamiliki wake wamejiunganishia maji ya Dawasa isivyo halali
Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla (kulia), akimhoji mchezaji wa zamani
wa Simba, Dua Said ambaye alikuwa miongoni mwa watu watano waliokamatwa
kwa tuhuma za kujiunganishia maji isivyo halali kutoka kwenye mabomba
ya Mamlaka ya Maji Safi na Taka (Dawasa), kwenye nyumba zao zilizopo
Bonde la Mto Msimbazi, Kigogo, Dar es Salaam. Makalla alikuwa kwenye
ziara ya kukagua miradi ya maji Dar es Salaam
Askari wakilinda doria katika eneo hilo
Moja ya malori yanayojazwa maji katika eneo hilo. Nalo liko chini ya ulinzi
Waziri Makalla akielezea athari zinazotokana na wizi huo wa maji ambapo
alisema kuwa katika nyumba hizo tano kila siku wanaiba maji lita laki
tatu, hivyo kila siku kuikoseasha serikali mapato ambapo kwa mwezi
yanafikia sh. bil 1.4.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akielezea jinsi
atakavyoshirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya ufisadi wa maji
jijini na kwamba atakuwa bega kwa bega kuhakikisha mswada wa adhabu
kubwa kwa wezi wa maji unapelekwa Bunge la Novemba mwaka huu.
Mchaezaji wa zamani wa Simba, Dua Said akielezea kwa wanahabari na
mbele ya Waziri Makalla, jinsi anavyoshirikiana na Shirika la Maji Safi
na Taka Dar es Salaam (DAWASCO), katika biashara ya kuuza maji. Dua Said
alikuwa ni miongoni mwa watu watano waliokamatwa kwa tuhuma za
kujiunganishia maji ya Dawasco isivyo halali katika eneo la Bonde la
Msimbazi
Bomba jipya la maji likitandazwa eneo la Makongo tayari kwa maandalizi
ya kusafirisha maji kutoka Mtambo wa Ruvu Chini ambao upanuzi wake
umekamilika hivi karibuni.
Makalla akiuliza swali kwa wakandarasi kuhusu utandazaji wa bomba hilo,
wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maji Dar na Pwani.
Waziri Makalla akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee,
Mwenyekiti wa CCM, Salum Madenge, (KUSHOTO) Deusdedit Mtiro (kulia)
walipokuwa wakimlaki alipowasili kwenye mkutano katika Kata ya Makongo.
WAFUASI WA CHADEMA WAKISHANGILIA NA KUMTAKA WAZIRI AWAHAKIKISHIE UPATIKANAJI WA MAJI MAKONGO JUU
Chadema na CCM wakishangilia katika mkutano huo
Waziri Makalla akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Makongo
Moja wa wananchi akilalamika mbele ya waziri kuhusu adha kubwa wanaipata ya maji eneo la Makongo juu
Msafara wa viongozi wa Chadema na CCM ukielekea kwenye mkutano wa
wananchi katika Kata ya Goba ambao hata hivyo ulivunjika baada ya
kutokea vurugu
WanaCCM wakimshangilia Waziri Makalla alipokuwa akihutubia wananchi katika Kata ya Makongo
Chadema wakishangilia wakati Halima Mdee akihutubia Makongo Juu
Mfuasi wa Chadema akilalama
Mdee akizungumza na wanahabari baada ya mkutano wa Kata ya Goba kuvunjika
Wana CCM WAKISEREBUKA
mNYIKA AKIZUNGUMZA NA WAFUASI WA cHADEMA BAADA YA MKUTANO KUVUNJIKA