WANANCHI WAKABILIWA NA UPUNGUFU MKUBWA WA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII MKOA WA ARUSHA.
Wananchi wa kata ya Sokoni 1 Mkoa wa Arusha wanakabiliwa na tatizo la upungufu wa zahanati pamoja na huduma muhimu za kijamii licha ya juhudi zinazofanywa na diwani wa kata hiyo kwakushirikiana na wahisani mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata hiyo Bw Michael Kivuyo wakati akiwasomema wananchi taarifa ya mwaka wananchi hao pamoja na kusomewa mapato na matumizi yatokanayo na fedha zinzotolewa na wahisani pamoja na wananchi.
Bw.Kivuyo amesema kuwa licha ya kufanikiwa kupunguza matatizo muhimu yaliyokuwa yakiwakabili wananchi,kwa kusaidiana na serikali pamoja na wahisani mbalimbali lakini kumekuwa na uhaba wa Zahanati za serikali na binfsi,Hospital pamoja na uhaba wa maji licha ya jitihada kufanyika.
Katika mkutano huo uliofanyika Katika kiwanja cha Shule ya Sinon Kilichopo maeneo ya Unga LTD Kata hiyo ya sokoni 1 Pia taarifa yay a maendeleo ya Elimu yamekuwa yakiridhisha Licha yakuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa pamoja matundu ya choo sambamba na utoro kwa wanafunzi.
Kwa upande wake Mtendaji wa Kata hiyo Bi Mari Lawrence Sirikwa wakati akiwasomea waanchi hao taarifa hizo kata hiyo imejitahidi kuimarisha ulinzi shirikishi na kuwafanya raia kuishi salama na mali zao pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika shughuli za kimaendeleo na kuunda vikundi ambavyo vinawazesha kujikwamua na umaskini.
Pamoja na hayo diwani wa kata hiyo Michael Kivuyo amesema kuwa wanahakikisha malengo yao waliyojiwekea ya kuhakikisha barabara zote za kata hiyo zinapitika wakatika wote kwakiwango cha lami.
Licha ya taarifa hizo kusomwa wananchi walipata fursa ya kuuliza maswali yao na kuweza kujibiwa na diwani huyo kwa ufasaha na hivyo kuwafanya wananchi kuridhika na taarifa hiyo.