Engineer
Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na
vyombo vya habari kuhusiana na Tamasha kubwa la upendo kwa mama
linalotarajiwa kufanyika jijini Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri
Abeid tarehe 02-11-2014
Engineer
Carlos Mkindi ambaye ni mkurugenzi wa mkundi production akiongea na
wanahabari kuhusiana na Tamasha la Upendo kwa mama ambalo linalenga
kutoa mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwawezesha
kujiajiri pamoja na kuwaombea na kuwashukuru kwa moyo wa upendo
waliyonayo kwa kujitoa katika kusimamia familia na malezi
Mratibu wa Tamasha la Upendo kwa mama Bw. Linus Kilembu akiongelea maandalizi ya Tamasha kuwa limekamilika kwa asilimia 90
Engineer
Carlos Mkindi mwenyekiti wa Tamasha la upendo ambaye ni mkurugenzi wa
mkundi production akifanyiwa mahojiano na wanahabari katika studio za
mkundi production zilizopo njiro mkoani Arusha
Kampuni
ya Makundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya
tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA
ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya
Sheikh Amri Abeid.
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili
wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku
likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester
Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline
Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na
Kwaya Mbalimbali.
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa
Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa
kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama
wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia
Familia na malezi ya watoto.
Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO
KWA MAMA wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo
yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali
ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA.
WAKINA MAMA WAPATA MKOMBOZI JIJINI ARUSHA.NI KATIKA TAMASHA LA INJILI LA 02/11/2014
Reviewed by
Unknown
on
10:44 AM
Rating:
5