Mtoa
habari aliyegoma kutaja jina amesema chanzo cha mgogoro huo na kifo cha
muumini ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondari KAGEMU ni baada ya
marehemu kuoa mwanamke wa dini nyingine (inaifadhiwa) na kumbadilisha
dini huyo mkewe na hapo waumini wa dini ya mkewe walianza vitimbwi kwa
kanisa hilo na hadi mauaji hayo kumekuwa na vurugu za kila mara baina ya
pande mbili.
Polisi
bado wanachunguza na watatoa taarifa baadae,mwili wa marehemu
umeifadhiwa katika chumba cha maiti bukoba mjini,majeruhi amelazwa
hospital ya mkoa.
Viongozi wa makanisa ya PAG walitarajiwa kutoa tamko rasmi mchana wa leo.