Header Ads

Okwi apigwa stop Simba

STRAIKA wa Simba, Emmanuel Okwi hatakuwepo kabisa kwenye kambi ya timu hiyo nchini Afrika Kusini kutokana na mechi mbili za timu yake ya Taifa ya Uganda ndani ya kipindi kifupi.
Lakini hiyo ikaushie, ishu ni kwamba uongozi wa Simba umethibitisha kwamba madaktari wameshauri mchezaji huyo asipande usafiri wowote wa majini kama wanayapenda maisha yake. Wameshauri atumie nchi kavu na angani tu.
Uchunguzi wa Mwanaspoti awali ulibaini kwamba Okwi tangu atue katika kikosi hicho msimu huu akitokea Yanga hakuwahi kupanda boti kama wachezaji wenzake wakati wakienda na kurudi kambini Zanzibar hali ambayo ilianza kuzua maswali kwa baadhi ya wachezaji kwamba Okwi anadekezwa zaidi na uongozi kwa kupewa huduma maalumu.
http://dewjiblog.com/wp-content/uploads/2014/09/Okwi.jpgHabari za ndani zinadai kwamba kumekuwa na minong’ono ya chini kwa chini baina ya wachezaji wakihoji hali hiyo bila majibu ingawa baadhi ya wakongwe waliwaridhisha kwamba labda suala la ndege ni makubaliano kwenye mkataba wake wa kazi.
Wachezaji waliocheza naye siku za nyuma walidai kwamba tangu atue Simba miaka ya nyuma usafiri wake ulikuwa ni ndege na aliwahi kujaribu maji akapata matatizo.
“Hao wanaoshangaa hawajui, watakuwa wageni lakini hata kama wageni hivi karibuni tuliwaambia kwamba siyo kipindi hiki tu hata huko nyuma Okwi alikuwa hapandi boti kutokana na kwamba aliwahi kupata matatizo mara moja alivyotumia usafiri huo,” alisema mmoja wa viongozi wakongwe na mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Simba kwa sasa.
Bosi wa Simba Tanzania nzima, Rais Evans Aveva alithibitisha kwamba Okwi hadekezwi ni hali halisi na ushauri wa daktari wanaufanyia kazi.
“Nikweli Okwi hatumii usafiri wa maji, hili si jambo geni ni la muda mrefu na tumekuwa tukilazimika atumie usafiri wa ndege kila tunapoelekea Zanzibar ikiwa ni sehemu ya ushauri wa madaktari ambao walitushauri, hivyo baada ya kubaini matatizo fulani kwa mchezaji wetu,” alisisitiza Aveva huku akiongeza kwamba hakuna mchezaji spesho Simba, wote ni sawa.
Powered by Blogger.