MKUNDI PRODUCTION YAANDAA TAMASHA KUBWA LA INJILI MKOANI ARUSHA.
KAMPUNI ya Mkundi Production ya jijini Arusha iko katika maandalizi ya kufanya tamasha kubwa la aina yake litakalo julikana kwa jina la UPENDO WA MAMA ambalo linatarajiwa kufanyika tarehe 02 Novemba 2014 katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid.
Tamasha hilo litaongozwa na waimbaji wa Nyimbo za Injili wakubwa kutoka Kenya, Sara K, na Cristina Shusho kutoka Tanzania, huku likipambwa na Ambwene Mwasongwe, Baraka Maasa, Eng calros Mkundi, Ester Bukuku, Matha Mwaipaja, Nesta sanga, Meth Chengula, Matumaini, Eline Patrick bila kuwasahau waimbaji wengine kutoka Mkoani Arusha pamoja na Kwaya Mbalimbali.
Aliyeandaa hili tamasha ndio huyu hapa wakuu, anaitwa Engineer Carlos Mkundi
Huyu
Lengo la tamasha hilo la UPENDO KWA MAMA linalengo la kutoa Mitaji kwa zaidi ya akina mama 50 wajasiriamali ili kuwaongezea uwezo wa kujiajiri, vilevile utakuwa ni wakati mwafaka wa kuwashukuru wakinamama wote kwa upendo waliyonao ukiambatana na kujitolea katika kusimamia Familia na malezi ya watoto.Studio ya Mkundi nakamati ya maandalizi ya Tamasha la UPENDO KWA MAMA Wanatoa nafasi kwa watanzania, Taasisi na Mashirika yote ambayo yako tayari kuungana na Studio ya Mkundi kwa Ufadhili wa hali na mali ili kufanikisha tamasha hili la UPENDO KWA MAMA
Ngoma hii hapa ya Engineer Carlos Mkundi anatarajiwa kutambulisha albam yake mpya.
Check moja ya video zake hapa ==>http://youtu.be/cQcVb0-YHHI
Aliyeandaa hili tamasha ndio huyu hapa wakuu, anaitwa Engineer Carlos Mkundi