Header Ads

SARAH K KUTOKA KENYA UPENDO NKONE,CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA KUWASHA MOTO NDANI YA JIJI LA ARUSHA TAREHE 02/11/2014.



 

Jiji Arusha hivi karibuni litakumbwa na Mkusanyiko mkubwa wa Wakazi wa Mkoa huyo pamoja na mikoa jirani Kuwashuhudia Waimbaji Mahiri wa nyimbo za Injili kutoka Nchini Kenya na hapa Tanzania ambao watahudumu katika Tamasha la Upendo kwa MAMA.


Tamasha hilo ambalo linatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Shek Amri Abed Arusha linatazamiwa kufurika mamia watu kutokana na waimbaji hao maarufu kuhudumu katika uwanja huo.

Hata hivyo wakazi wengi wa jiji la Arusha wamedai kutokukosa katika Tamasha hilo ambalo ni maususi kwa watu wote wenye rika tofauti kwaajili ya kuonyesha upendo kwa wakina MAMA ambapo pia wakina mama wataweza kupatiwa misaada mbalimbali ili kujikimu kimaisha.

Hii itakuwa ni mara ya Kwanza kwa wasanii wa nyimbo za Injili Wakiwa chini ya Usimamizi wa Kampuni ya MKUNDI PRODUCTION ya jiji Hapa, kuweza kuandaa Tamasha kubwa na lenye kuteka hisia za watu wengi ambalo ni kwaajili ya kuwasaidia wakina MAMA.

Watakao kuwepo katika Tamasha hilo ni pamoaja na UPENDO NKONE CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA,SARAH K KUTOKA KENYA,ENG CARLOS MKUNDI,BARAKA MASSA,ESTER BUKUKU,NESTER SANGA,MESS CHENGULA,FLORA MWENDA PAMOJA NA MATUMAINI NAYE ATAKUWEPO SIKU HIYO.
Powered by Blogger.