NIWAKATI AMBAO ULIKUWA UKISUBIRIWA KWA HAMU!TAMASHA KUBWA LA INJILI.ARUSHA,CHRISTINA SHUSHO,MARTHA MWAIPAJA,UPENDO NKONE,ENG CARLOS MKUNDI,SARAH K NA WENGINE WENGI WATAACHILIA UPAKO WA HALI YA JUU.
Tamsha hilo lenye lengo la kuwaenzi wakina mama kwakuonyesha umuhimu wake katika jamii na familia kiujumla,limeandaliwa na Kampuni inayohusika na uandaaji wa matamasha mbalimbali,Music,pamoja na utengenezaji wa matangazo Kampuni ya Mkundi Production Iliyopo Jijini Arusha Maeneo ya Njiro PB.
Kuonyesha kuwa Tamasha hilo linashura na muonekano wa Kitofauti Litahudhuriwa na Wasanii mbalimbali wa nyimbo za Injili Kutoka Tanzania na Nchini Kenya.
Wasanii hao ambao watakuwepo ni pamoja na Martha Mwaipaja,Upendo Nkone,Christina Shusho,Sarah K.Eng Carlos Mundi,Baraka Massa,na wasanii wengi ambao watakuwepo katika tamasha hilo ambalo nlinatarajiwa kufanyika tarehe 02/11/2014 katika Uwanja wa Shekh Amri Abed Jijini Arusha.
Hata hivyo mwitikio wa Tamasha hilo umeonekana kupokelewa kwa hisia kubwa kwani watu wengi wameahidi kuhudhuiria siku hiyo.