Header Ads

JAMII YA ASWA KUWAENZI MAMA ZAO NA KUACHA MTAZAMO POTOFU



Katika kuhakikisha kila mtu anawaenzi na kuwaheshimu wazazi wao hasa MAMA jamii imeshauriwa kuwajali na kuwapenda na kutambua kuwa kila mtu aliletwa na mama hapa duniani.

Hayo yamesemwa na Rais wa Upendo Kwa Mama Foundation Eng:Carlos Mkundi wakati akizungumzia uzinduzi wa msimu mpya wa matamsha ya Upendo kwa Mama kwa mwaka 2015,ambalo litazinduliwa Rasmi na  Mh Mwigulkulu Nchemba Jiji Dar Mwaka mpya.
Carlos amesema imefika wakati jamii kubadilisha mtazamo wao wa kutokuwajali Mama zao na kutambua kuwa wanao mchango mkubwa sana kwa wao kuja Duniani.
Amesema kuwa lazima watu wakabadilika kutokana na mambo ambayo yanawakuta wakina mama yakiwemo kunyanyaswa na jamii na kutengwa na kuona kama hawana msaada.
Pia amesema waathirika wengi wa matukio ya kiukatili ni wakina mama hivyo kuna kila sababu ya kuwakomboa Kiuchumi na Kiroho Pia.
Sambamba na hayo ameeleza sababu za yeye kuamua kuanzisha Upendo Kwa Mama Foundation kuwa ni kutokana na kuona wakina mama wanavyo nyanyasika kwakuombaomba pamoja na kutokuwa na nafasi katika familia.
Hivyo kutokana  na hayo sehemu wa mapato wanayoyapata kupitia matamsha mbalimbali wanayoyafanya nchini unaingizwa katika mfuko maalumu wa Upendo Mama Foundation.
Uzinduzi huo utaenda sambamba na Utambulisho wa Albamu yake mpya Inayojulikana kwa jina la WEWE NI MUNGU.na litahudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kiserikali na Taasisi binafsi
Powered by Blogger.