MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA MJINI AINGIA MATATANI
Mwenyekiti wa Chadema Iringa Mjini |
MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Iringa Mjini, Frank Nyalusi
ameingia matatani baada ya kudaiwa kutoa tuhuma zisizo za kweli dhidi ya Kamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi
(UVCCM) Mkoa wa Iringa, Salim Asas, kwa lengo la kujipatia umaarufu.
Katika
mkutano
wa hadhara uliofanywa na Chadema hivikaribuni kwenye uwanja wa
Mwembetogwa
mjini Iringa, Nyalusi ambaye pia ni diwani wa kata ya Mivinjeni mjini
Iringa, anadaiwa kutoa tuhuma zinazowahusisha vijana watatu ambao
hata hivyo hakuwataja majina; kwamba walitumwa na Kamanda huyo wa UVCCM
kwenda
kumdhuru.
Taarifa
za uhakika zilizoufikia mtandao huu zimedai Asas kwa kupitia wakili wake, Alfred
Kingwe amekwisha mkabidhi Nyalusi hati ya madai (Demand Note) inayomtaka kukanusha
tuhuma hizo ndani ya siku 14 vinginevyo atafikishwa mahakamani.
Kwa
kupitia hati hiyo ya madai Nyalusi anatakiwa kuitisha mkutano katika eneo lile
lile alilotolea tuhuma hizo na kukanusha madai hayo yanayoelezwa kupikwa kwa
lengo la kuchafua wasifu wa Asas na kumuongezea Nyalusi umaarufu.
Katika
kumnurusu Nyalusi dhidi ya mkono wa sheria endapo atashindwa kuitisha mkutano
huo, baadhi ya viongozi wa chama hicho wanadaiwa kumpigia magoti Bwana Asas ili
suala hilo limalizwe kiungwana.
Mmoja
wa viongozi wa chama hicho, Abou Changawa alisema; “tunamtafuta Bwana Salim,
tunajua ni muungwana, tunataka suala hili tulimaze kiungwana; kama
itashindikana kuitisha mkutano wa hadhara basi tutafanya mkutano na waandishi
wa habari ili kuiweka sawa taarifa hiyo.”
Mtandao
huu utaendelea kukujuza kinachoendelea kuhusiana na habari hii.....