ZIJUE SABABU ZA NYALANDU ATANGAZA KUWANIA URAIS......!
Mbunge wa
Singida Kaskazini, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu
ametangaza rasmi kuwania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu mwakani.
Amesema
amechukua uamuzi huo baada ya kuona kwamba anao uwezo wa kuiongoza
Tanzania, katika harakati za kuwafikisha kwenye maendeleo endelevu
wanayotaka Watanzania.
Amesema,
yuko tayari kushindanishwa na Watanzania wengine watakaoona kuwa wanafaa
kuwa Rais, lakini akisema kwanza kila atakayejitokeza itabidi kazi zake
zipimwe kwa moto na endapo zitayeyuka hafai.
Nyalandu
ambaye alitangaza uamuzi huo kwenye Uwanja wa Michezo wa Ilongelo jimbo
la Singida Kaskazini, alisema, yeye anaingia kwenye kinyang'anyiro akiwa
kifua mbele kutokana na kuamini kwamba amekwishafanyakazi zilizotukuka.
"Kazi
zangu nilizofanya zinajulikana na ninaziamini kwamba ni nzuri, hivyo
yeyote atakayetaka urais apimanishwe na mimi kwa kupimwa kazi zetu kwa
moto", alisema Nyalandu
Itakapofika
siku ya siku, nitaenda Dodoma nikisindikizwa na wana Singida Mashariki,
na wengine wengi kutoka pembe zote za Tanzania, kwenda Dodoma kuchukua
fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Urais kwa tiketi ya CCM",VICTOR SIMON