NYALANDU: HATUNA MPANGO KUFUKUZA WAMASAI LOLIONDO
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akijaribu kurusha
mkuki alipotembelea eneo la Loliondo wilayani Ngorongoro kukanusha uvumi
juu ya kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiagana na mzee
wa kimasai mara baada ya kumaliza mkutano uliokuwa na lengo la kukanusha
uvumi juu ya kuondolewa kwa jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Raphael
Rong’oi akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai kabla ya
kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu (aliyekaa
kwenye pikipiki).
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiwa katika picha
ya pamoja na baadhi ya wanawake wa jamii ya kimasai mara baada ya
kumaliza mkutano nao.
Wamasai wakichukua kumbukumbu muhimu katika mkutano wao na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akiongea na
Wamasai waliokusanyika kwa ajili ya kusikia tamko la serikali juu ya
uvumi wa kuondolewa kwa Jamii ya Wamasai katika eneo hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu akionja maji
kutoka katika kisima kilichojengwa kwa ajili ya kutatua tatizo la maji
katika katika eneo la Loliondo.
Novemba mwaka huu, gazeti The Guardian la nchini Uingereza, liliandika habari kuwa serikali ina mpango wa kuwafukuza Wamasai wanaoishi eneo hilo.
Gazeti hilo lilidai kuwa, lengo ni kuwapatia eneo lenye kilometa za mraba 1,500, kampuni ya OBC ya Falme za Kiarabu.
Akizungumza na wananchi wa jamii ya kimasai wilayani Ngorongoro mwishoni mwa wiki, Nyalandu alisema habari hizo hazina ukweli wowote isipokuwa zina lengo la kuchafua taswira nzuri ya nchi yetu kimataifa.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kuishi bila hofu, kwa sababu serikali haina mpango wa kuwaondoa kwenye makazi yao.
“Nami niwahakikishie wanajamii wa Loliondo, Ngorongoro na wanajamii wote wa kimasai ambao wametishiwa nyau, kuwa serikali ya Tanzania haina mpango wowote wa kumfuata na kumfukuza mtu yoyote,” alisema.