Header Ads

Hatimaye Kesi ya Daudi Mwangosi Yapandishwa Kizimbani na Hichi Ndicho Kilichoamuliwa


Marehemu Daudi Mwangosi
 Mahakama Kuu kanda ya Iringa inaendelea na vikao vyake huku leo kesi ya ya mauwaji ya mwanahabari mkoani Iringa Daud Mwangosi inayomkabilia mtuhumiwa wa askari wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoa wa Iringa (FFU) Pasificus Cleophace Simon mwenye namba G 2573 inataraji kuanza kusikilizwa kwa upande wa mashahidi kuanza kutoa ushahidi wao.
Polisi wakiwa wanamshambulia Daudi Mwangosi

Kesi hiyo  iliyoanza Feb 12  mwaka huu huenda hukumu ya kesi hiyo kutolewa siku ya tarehe 18 mara baada ya mashahidi kumaliza kutoa ushahidi wao ama kuendelea kikao kijacho iwapo mashahidi wote zaidi ya 17 waliopo katika kesi hiyo watashindwa kufika mara ya mwisho mtuhumiwa huyo kusomewa makosa yake mwaka jana.

Kushoto ni Polisi anaedaiwa kumuua Daud Mwangosi
Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo kwa gari la kifahari lenye namba za kiraia T 320 ARC linalosadikiwa kuwa ni la RCO huku kwa mara ya pili akifikishwa kwa miguu na kuondolewa mahakamani hapo kwa gari namba DFP 2175 pick up akiwa katika ulinzi mkali huku waandishi wa habari wakidhibitiwa na polisi na mmoja wao kunusurika kupigwa.

Katika kesi hiyo hali ya kutofahamu imekuwa ikijitokeza na kufanya watu kuwa na maswali zaidi baada ya 14 Februari Mwaka jana mtuhumiwa huyo mwenye namba G 2573 akiwa mahakamani hapo aliwatukana waandishi wa habari matusi ya nguoni kuwataka wasimpige picha huku akijidai kuwa muda si mrefu ataachiwa na kupambana na waandishi mitaani.

Siku hiyo(Februari 14,2012) Pasificus akiwa na jazba alisikika akisema.

“mtapiga picha sana mtakavyo lakini hamjui kama kesho tu nitatoka halafu tupambane mitaani huko. Nawaona sana mnaonipiga picha tutakuja kukutana tu” alisema mtuhumiwa huyo.
Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2 mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi alipokuwa akiwajibika kwa kazi za kihabari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA). 
Powered by Blogger.