Mbowe aiyomba serikali kuondoa zuio la mikutano ya siasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mheshimiwa FREEMAN MBOWE ameitaka serikali kubadili uamuzi wa kuzuia mikutano na shughuli nyingine za siasa kwa kuwa Tanzania ilishakubali na kuingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza
na wananchi kwenye mkutano wake wa kumnadi mgombea wa udiwani katika Kata ya
Kitwiru Manispaa ya Iringa,Mheshimiwa MBOWE amesema serikali iliyopo madarakani
imechaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano hivyo inapaswa kuheshimu
sheria pamoja na katiba hiyo ikiwemo sheria namba tano iliyorejesha mfumo huo
mwaka 1992 kabla ya hapo awali kufutwa mwaka 1965.
Mbunge
wa Iringa Mjini Mchungaji PETER MSIGWA amewataka wananchi wa Kata ya Kitwiru
kuchagua mgombea wa CHADEMA ili aongeze nguvu kwenye baraza la madiwani
linaloongozwa na chama hicho ambalo limeifanya Manispaa ya Iringa kuwa mfano wa
kuigwa katika mambo mengi ya uendeshaji halmashauri nchini.
Kwa
upande wake Mgombea wa udiwani kupitia chama hicho,Bwana BAHATI CHENGULA amewataka
wananchi kuendelea kumwamini kama walivyomwamini awali na kumchagua kuwa
Mwenyekiti wa mtaa ,kazi ambayo ameifanya kwa uadilifu na kujituma kwa lengo la
kusukuma mbele maendeleo yao.