BETHDEI-RYAN GIGGS NI MIAKA 40, NI LEJENDARI LAKINI BADO NI SUPASTAA, UWANJANI!!
>> GEORGE BEST, LEJENDARI WA MAN UNITED, ALISEMA: "IPO SIKU WATU WATASEMA MIE NILIKUWA RYAN GIGGS MWINGINE!"
>>RON ATKINSON: ‘GIGGS ANAKUFANYA UAMINI KUNA MUNGU WA SOKA!‘
JUZI,
ndani ya BayArena, Jijini Leverkusen, ambako Bayer Leverkusen ni ngome
yao na haifungiki hapo, Ryan Giggs, akiwa amebakisha Siku 2 tu kutimiza
Umri wa Miaka 40, alikiongoza Kikosi cha Manchester United
kilichoiteketeza Bayer Leverkusen Bao 5-0 na kufuzu kutinga Raundi ya
Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Leo hii, Ryan Giggs, Mchezaji anaeongoza
Uingereza kwa kutwaa Mataji na Medali lukuki, bado anachanja mbuga
Uwanjani na leo hii ametimiza Miaka 40 akiwa bado ni Mchezaji wa
Mabingwa wa England, Manchester United, ingawa Msimu huu ana wadhifa
mwingine pia wa kuwa ni mmoja wa Makocha wa Timu hiyo.
Giggs, ambae alianza kuichezea Man
United tangu Mwaka 1990, akicheza Mechi zaidi ya 1,000 kwa Miaka
takriban 23 na kutwaa Makombe 34, amesema: “Nitafurahi hii ikipita. Hii
ni wazi ni kumbukumbu lakini siifikirii sana na kweli sikumbuki hadi
Watu waniambie.!!”
TUKISHEHEREKEA SIKU HII YA GIGGS, NI BORA KUKUMBUKA NINI WACHEZAJI MAGWIJI WAMEZUNGUMZA KUHUSU YEYE:
- ALESSANDRO DEL PIERO, Mchezaji wa zamani wa Juventus na Italy: “Ni Wachezaji wawili tu hunifanya nilie nikitazama Soka. Mmoja alikuwa Diego Maradona na mwingine Ryan Giggs”
-ZINEDINE ZIDANE, Mchezaji wa zamani wa Real Madrid, Juventus na France: “Wote tuliokuwa Juventus tulikubali Man United ndio Klabu Bora tuliyokutana nayo Ulaya na Ryan Giggs ni kiwango cha Dunia!’’
PEDRO WA BARCELONA:
"Yeye ni Lejendari ambae bado anaishi. Na kwa Mtu kama mimi kucheza nae,
ambae nimekua nikimuona anacheza, ni furaha na heshima kubwa!”
SIR ALEX FERGUSON, MENEJA MSTAAFU WA MAN UNITED: “Ni Mchezaji Bora na Binadamu wa ajabu sana!”
WAYNE ROONEY, STRAIKA WA MAN UNITED NA ENGLAND: “Ryan anashangaza. Nguvu yake Uwanjani, Pasi zake na jinsi anavyohangaika, huwezi kuamini. Ni heshima kubwa kucheza nae!”
RIO FERDINAND: “Nadhani
akitundika Daluga juu, ndipo Watu watagundua ni aina gani ya Mchezaji
wa ajabu alivyokuwa na mafanikio ya ajabu aliyopata!”
TOM CLEVERLY, KIUNGO WA MAN UNITED NA ENGLAND, AMENENA: “Sikumbuki nilikuwa na Umri gani wakati najidai mie ndie Ryan Giggs kwenye bustani nyuma ya Nyumba yetu!”
GARY PALLISTER, BEKI WA ZAMANI WA MAN UNITED: “Wakati Ryan Giggs akikimbia na Mpira, Damu za Wachezaji Wapinzani zilipinda! ”
GEORGE BEST, LEJENDARI WA MAN UNITED, ALINENA: "Ipo Siku moja Watu watasema mie nilikuwa Ryan Giggs mwingine!"
BRIAN KIDD, MENEJA MSAIDIZI WA ZAMANI WA MAN UNITED: “Kipaji chake ni hulka ya Mungu. Atabaki na Kipaji chake hata akistaafu!”
BEKI WA ZAMANI WA ARSENAL, MARTIN KEOWN: “Ni kitu adimu kwa Mtu mmoja kuchezea Klabu moja kwa muda mrefu!”
+++++++++++++++++++++++++++++++++
TULIITOA HII NYUMA:
LEJENDARI GIGGS: 2 MACHI 1991-2 MACHI 2013, MIAKA 22 LIGI, MECHI 1000!!!
Friday, 01 March 2013 10:39
>>RON ATKINSON: ‘GIGGS ANAKUFANYA UAMINI KUNA MUNGU WA SOKA! ‘
>>GEORGE BEST: ‘IPO SIKU WATU WATASEMA MIE NILIKUWA GIGGS MWINGINE!!’
TAREHE 2 MACHI 1991, ndio aliingizwa
toka Benchi kucheza Mechi yake ya kwanza ya Ligi ya Manchester United
dhidi ya Everton na Jumamosi, Tarehe 2 Machi 2013, atatimiza Mechi yake
ya 1000 kama atapewa Namba kucheza dhidi ya Norwich City kwenye Mechi ya
Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.
Aliemgundua Ryan Giggs ni Wakala wa
Magazeti na ambae pia alikuwa Mlinzi wa Old Trafford, Harold Wood,
aliemdokeza Alex Ferguson kuhusu Chipukizi huyo na Ferguson akatuma Mtu
kwenda kuchunguza na hatimae Giggs akapewa Majaribio na Man United
Krismas ya Mwaka 1986.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
GIGGS NDIE MWENYE REKODI UINGEREZA KWA MATAJI MENGI:
-UBINGWA LIGI KUU: 13
-FA CUP: 4
-LIGI CUP: 3
-CHAMPIONZ LIGI: 2
-NA MENGINE MENGI!!!
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
SIR ALEX FERGUSON:
-Nakumbuka mara ya kwanza
kumuona, alikuwa na miaka 13 na alikuwa akielea kama ndege mdogo angani
anaekimbiza karatasi kwenye upepo!
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya hapo, Giggs, akiwa na Miaka 13
tu, aliongoza Timu yake Salford Boys kucheza na Kikosi cha Vijana wa
chini ya Miaka 15 cha Man United na alipiga hetitriki huku Ferguson
akiwa kwenye Dirisha la Ofisi yake akishuhudia.
Alipotimiza Miaka 14, Tarehe 29 Novemba
1987, Sir Alex Ferguson, alikwenda Nyumbani kwa kina Giggs na kumpa Ofa
ya kusainiwa kwa Miaka miwili kama Mchezaji Chipukizi Mwandamizi toka
Shuleni.
HAPO NDIO HISTORIA INAYOENDELEA ILIPOANZA…………………..
NINI WANASEMA JUU YAKE:
-MARTIN KEOWN: Nilipomwona mara ya kwanza akicheza alikuwa Mtoto, mwembamba sana …sasa Lejendari!!
-ALESSANDRO DEL PIERRO: Ni Wachezaji wawili tu hunifanya nilie nikiwaona wakicheza, mmoja ni Diego Maradona na mwingine Ryan Giggs!!
-JOHAN CRUYFF: Eric Cantona ni Mchezaji Bora lakini hamfikii Ryan Giggs!!
-BRIAN KIDD: Kipaji chake amepewa na Mungu. Atabakia na Kipaji hicho hicho hata kama atastaafu kwa sababu kipaji aina hii hakitoweki!!
-RON ATKINSON: Giggs anakufanya uamini kuna Mungu wa Soka!
-GEORGE BEST: Ipo Siku Watu watasema mie nilikuwa Giggs mwingine!!
-PAUL SCHOLES: Wapo Wachezaji Bora sana nimecheza nao Timu moja lakini kama kuchagua Bora ni Giggs, anaweza kufanya chochote!!
-FERGUSON: Ryan anaweza kuwafanya Mabeki Damu zao zipinde!!