HAZARD AMTAKA KEVIN DE BRUYNE AHAME CHELSEA!!
KATIKA
hatua ya kushangaza, Winga wa Chelsea na Belgium, Eden Hazard, amemtaka
Mchezaji mwenzake wa Klabu hiyo na pia Belgium, Kevin De Bruyne, ahame
Chelsea.
Ushauri huo wa Hazard umetolewa kwa De
Bruyne, ambae ndie Mfungaji Nambari Wani wa Timu ya Taifa ya Belgium
wakati wa Mechi za Kundi lao la Ulaya la Kombe la Dunia ambalo wamefuzu
kucheza, ili kumwokoa apate namba kwenye Fainali za Kombe la Dunia za
Mwezi Juni Mwakani huko Brazil.
De Bruyne, ambae alipelekwa Mkopo huko
Werder Bremen ya Germany Msimu uliopita, Msimu huu ameanza Mechi 4 tu za
Chelsea na hakumaliza hata moja.
Alhamisi iliyopita, Belgium walicheza
Mechi ya Kirafiki na Colombia, na De Bruyne, mwenye Miaka 22, alicheza
Mechi hiyo huku mmoja wa Watazamaji akiwa Meneja wa Chelsea Jose
Mourinho.
Binafsi De Bruyne amekiri ni bora aende
kwa Mkopo Klabu nyingine ili aongeze nafasi yake kuwemo Kikosi cha
Belgium kitakachocheza huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia na
Hazard ameunga mkono hilo.
Akiongea na TV ya Belgium, Hazard
alisema: “Hakika, kucheza Kombe la Dunia bila kucheza Mwaka mzima ni
ngumu. Bora aondoke Chelsea na kwenda kucheza. Kama tunataka kupata
ubora wa Kevin, ni bora aondoke!”
Moja ya Klabu za Bundesliga huko Germany
ambazo zinatajwa kumwinda De Brutne ni Schalke ambayo Meneja wao, Jens
Keller, amekiri kuvutiwa na Mchezaji huyo.
Keller amelambia Gazeti la Bild: “Kevin de Bruyne ni Mchezaji mzuri sana, ana kipaji kikubwa!”