KOMBE LA DUNIA-BRAZIL 2014: 8 ZA MWISHO KUJULIKANA JUMANNE & JUMATANO!
AFRIKA BADO 2, ULAYA 4 & MECHI ZA KIMATAIFA MCHUJO 2!!
Afrika imebakisha Nafasi 2, Bara la
Ulaya 4 na Nafasi 2 zitatokana na Mechi za Kimataifa mbili za Marudiano
kati ya New Zealand na Mexico, huku Mexico wakiwa mbele kwa Bao 5-1, na
nyingine kati ya Uruguay na Jordan huku Uruguay wakiwa kifua mbele kwa
Bao 5-0.
Kwa Afrika, ambako Wikiendi hii Nchi 3
zilifuzu ambazo ni Mabingwa wa Afrika Nigeria, Ivory Coast na Cameroun,
zipo Mechi mbili zitakazotoa hizo Timu mbili za mwisho.
Algeria, ambao walifungwa 3-2 na Burkina
Faso, wako kwao kurudiana na Timu hiyo na Egypt wako Mjini Cairo
kujaribu kupindua kipondo cha 6-1 walichopewa na Ghana.
Huko Ulaya, zipo Mechi 4 za Marudiano ambazo zitatoa Timu 4 kuungana na 9 toka Bara hilo ambazo zimeshafuzu.
Croatia na Iceland zitatinga Uwanjani huku ngoma ikiwa Droo 0-0.
Sweden wako nyumbani kuivaa Portugal iliyowafunga Bao 1-0 kwa Bao la Cristiano Ronaldo.
Ukraine wanasafiri kwenda Stade de Paris
kurudiana na France waliyoichapa 2-0 huko Kiev na Greece wanatinga
Bucharest kuivaa Romania waliyoichapa 3-1.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA-KOMBE la DUNIA
Ulaya
MECHI za MARUDIANO
Jumanne Novemba 19
[Saa za Bongo]
SAA |
MJI |
MECHI YA KWANZA |
||
2115 |
Zagreb |
Croatia |
Iceland |
0-0 |
2145 |
Solna |
Sweden |
Portugal |
0-1 |
2300 |
Paris |
France |
Ukraine |
0-2 |
2100 |
Bucharest |
Romania |
Greece |
1-3 |
**WASHINDI WANNE WA MECHI HIZI ZA MARUDIANO WATATINGA BRAZIL KWENYE FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++
AFRIKA
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Novemba 19
Marudiano:
[Saa za Bongo]
[Katika Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
19:00 Egypt v Ghana [1-6]
21:15 Algeria v Burkina Faso [2-3]
**FAHAMU: Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
++++++++++++++++++++++++++++
MECHI ZA MCHUJO ZA KIMATAIFA:
Nov-20 |
0900 |
Wellington |
New Zealand |
Mexico |
CONCACAF/Oceania [1-5] |
Nov-21 |
0200 |
Montevideo |
Uruguay |
Jordan |
Asia/South America [5-0] |
++++++++++++++++++++++++++
TIMU AMBAZO ZIMEFUZU KWENDA BRAZIL
[Jumla 24 Bado 8]:
Afika [Nchi 3 Bado 2]: Nigeria, Ivory Coast, Cameroun
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA
Oceania[New Zealand wapo kwenye Mchujo]
**FAHAMU:
-RATIBA IMESHATOKA BOFYA HAPA: http://www.sokainbongo.com/kombe-la-dunia-brazil-2014
- DROO YA KUPANGA MAKUNDI:
-KUFANYIKA TAREHE 6 DESEMBA 2013 Costa do SauÃpe Resort, Mata de São João, Bahia, Brazil
-Kwenye Droo hiyo Timu 7, pamoja
na BRAZIL, ambazo ziko juu kwenye Listi ya FIFA ya Ubora Duniani
zitawekwa Chungu Na 1 na Timu nyingine 24 zilizobakia zitagawanywa nane
nane na kuingizwa Vyungu vingine vitatu na kutenganishwa kutoka Mabara
zinakotoka.
-FAINALI KUCHEZWA: 12 Juni 2014 hadi 13 Julai 2014
++++++++++++++++++++++++++