KOMBE LA SHIRIKISHO: TP MAZEMBE YASHINDA LAKINI BINGWA CS SFAXIEN!!
MBWANA SAMATTA APIGA BAO LA PILI!!
KLABU ya Tunisia CS Sfaxien leo imetwaa Taji lao la 3 la Kombe la Shirikisho huko Lubumbashilicha ya kuchapwa Bao 2-1 na TP Mazembe.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
MAGOLI:
TP Mazembe 2
-Cheibane Traore Dakika ya 10
-Mbwana Ally Samata 23
Club Sportif Sfaxien 1
-Fakhreddine Ben Youssef Dakika ya 88
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
CS Sfaxien wametwaa Kombe baada ya
kushinda Mechi ya kwanza Bao 2-0 iliyochezwa Jumamosi iliyopita kwenye
Mji wa Sfax Nchini Tunisia na hivyo kuvikwa Ubingwa kwa Jumla ya Mabao
3-2.
Sfaxien wameshatwaa Kombe hili Mwaka 2007 na 2008 na 2010 walikuwa Washindi wa Pili.
Kwa kutwaa Kombe hili, CS Sfaxien
wamezawadiwa Dola 660,000 na Mwezi Februari watacheza na Al Ahly ya
Egypt kuwania CAF Super Cup.