MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA TAMASHA LA 11 KWA ASASI ZA KIRAIA, JIJINI DAR LEO
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia washiriki wa Tamasha la 11 la Asasi za Kiraia, wakati alipokuwa akifungua rasmi Tamasha hilo katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, leo.
Rais wa Asasi za Kiraia, John Ulanga, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha, hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za Kiraia, Olive Luena,akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo.
Baadhi ya washiriki wa Tamasha hilo kutoka mikoa mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Tamasha hilo.
Baadhi ya washiriki wa Tamasha hilo kutoka mikoa mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Tamasha hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizindua rasmi Kitabu cha Asasi za Kiraia, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 11 kwa Asasi za Kiraia, uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza,jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Rais wa Asasi za Kiraia, John Ulanga (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Asasi za Kiraia, Olive Luena.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibofya kitufye kuashiria kuzindua rasmi Tovuti ya Asasi za Kiraia, wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 11 kwa Asasi za Kiraia uliofanyika kwenye Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi wa kukabiliana na ugonjwa Kansa nchini, Kisa Mwakatobe, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho, baada ya kufungua rasmi Tamasha la 11 kwa Asasi za Kiraia, uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Chama cha Albino Tanzania, Mohamed Chanzi (katikati) na Mzawa Jagane, wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho, baada ya kufungua rasmi Tamasha la 11 kwa Asasi za Kiraia, uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo.
Makamu
wa Rais, Dkt.Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi
wa Asasi za Kiraia, baada ya kufungua rasmi Tamasha hilo leo.(PICHA NA
OMR)