MESSY MAJERUHI TENA
NI MARA YA 3 MSIMU HUU, MESSI MAJERUHI!
LICHA
ya Mabingwa wa Spain, FC Barcelona, kuichapa Real Betis Bao 4-1 na
kuzidi kupaa kileleni mwa La Liga wakiwa Pointi 3 mbele ya Timu ya Pili
Atletico Madrid, wasiwasi mkubwa umetanda huko Nou Camp baada ya Nyota
wao Lionel Messi kulazimika kutoka katika Kipindi cha Kwanza.
Hii ni mara ya tatu kwa Msimu huu kwa
Messi kuumia huku ikidaiwa tatizo lake ni lilelile, Musuli za Pajani
[Hamstring], na Barca imethibitisha Staa huyo atafanyiwa uchunguzi zaidi
hii leo.
Mbali ya pigo hilo, Barca walipata Goli zao kupitia Neymar, Pedro na Cesc Fabregas aliefunga Bao 2.
Real Betis walifunga Bao lao katika
Dakika ya 90 kwa Penati ya Jorge Molina na kumaliza Mechi kwa kipigo cha
4-1 kilichowabakisha mkiani mwa La Liga.
Nao wapinzani wa Barca ambao wapo Nafasi
ya Pili na wamekuwa wakiwafukuza tangu mwanzoni mwa Msimu, Atletico
Madrid, walitoka Sare ya 1-1 huku Bao zote kwenye hii Mechi zikiwa ni za
kujifunga wenyewe.
Mario Gaspar alijifunga katika Dakika ya
Pili na kuipa Atletico Bao lao lakini katika Dakika ya 79, Juanfran
alijifunga na kuifanya Gemu imalizike 1-1.
Jumamosi, Real Madrid iliwachapa Real
Sociedad Bao 5-1 na Cristiano Ronaldo kupiga Hetitriki ikiwa ni
Hetitriki yake ya 23 kwa Real Madrid.
++++++++++++++++++
LA LIGA
MSIMAMO-Timu za Juu:
[Kila Timu imecheza Mechi 13]
1 FC Barcelona Pointi 37
2 Atletico de Madrid 34
3 Real Madrid CF 31
4 Villarreal CF 24
5 Athletic de Bilbao 23
6 Getafe CF 20
++++++++++++++++++