Mwenyekiti wa
Washirika wa Maendeleo Balozi wa Sweden , Lennarth Hjeimaker
(kulia)akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano wa
kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS)
ulioshirikisha na Washirika wa Maendeleo(DPS) na wadau mbalimbali
kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dares Salaam (kulia) Naibu Waziri wa Fedha Saada
Mkuya Salum .
Na Magreth Kinabo
Serikali
imesema kwamba itaendelea kuelekeza rasilimali katika
masuala ya elimu, afya, kilimo ikiwa ni hatua ya kuweza kupunguza
umasikini kwa haraka ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto
zilizopo katika sekta mbalimbali .
Kauli
hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum
wakati akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu mkutano
wa mwaka 2013 wa kupitia utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali (GBS)
ulioshirikisha na Washirika wa Maendeleo(DPs) na wadau mbalimbali
kutoka serikalini uliofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu J.K.
Nyerere jijini Dares Salaam.
“Changamoto
inayotukabili ni kuleta maendeleo kwa haraka. Uchumi wa nchi unakuwa
kwa asilimia 7 lakini umasikini umepungua kwa asilimia 2,”alisema Waziri
huyo.
Alisema changamoto
inayoikabili serikali ili kukabiliana na umasikini nchini ni
kuhakikisha inaelekeza rasilimali zake ili ziweze kuzalisha ajira
.Pia kuangalia idadi ya watu kulingana na uchumi wa nchi.
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri huyo kufuatia Mwenyekiti wa
Washirika wa Maendeleo Balozi wa Sweden ,
Lennarth Hjeimaker kueleza kuwa hatua
za kupunguza umasikini na upatikanaji wa huduma za jamii bado ni
ndogo ,kiwango cha ufaulu kwa shule za sekondari na msingi kushuka
na uwiano wa walimu na wanafunzi bado mdogo, zaidi ya nusu ya watu
vijijini wahapati maji safi na salama na upatikanaji wa nishati vijijini
bado ni changamoto.
Wadau hao pia wameishauri Serikali kuendelea kupambana na tatizo la rushwa nchini.
Katika
kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2012/2013 wadau hao walichangia
Dola za Marekani milioni 560 na mwaka huu wa fedha waliahidi kutoa Dola
za Marekani milioni 561 hivyo hadi sasa Serikali imeshapokea Dola za
Marekani milioni 290.2.
.............................
|