WANAFUNZI WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA (A.J.T.C)WAELIMISHWA KUHUSU MAAMBUKIZI YA UKIMWI.
Wanafuzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari na utangazaji Arusha (A.J.T.C) wakisikiliza kwa makini mada iliyo wasilishwa na wanafunzi waenzao kuhusiana na virusi vya ukimwi. |
Wanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari na utangazaji
Arusha wametakiwa kufahamu chanzo cha maambukizi ya ukimwi ili kuweza
kuwaelimisha jamii kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi mapya ikiwa ni moja
ya wajibu wao katika kuelimisha jamii.
Elimu hiyo imetolewa leo katika ukumbi wa chuo hicho na
wanafunzi wa darasa la Selous ambao ni wakwanza kutumia mtaala mpya unaoendana
na mfumu wa digital uliotambulishwa na baraza la habari nchini ili kuweza kukidhi vigezo vya taaluma hiyo ya
uandishi wa habari hapa nchini.
Mumo huo wa digitali unawalazimu wafunzi wa fani hiyo ya
uaandishi wa habari kusoma masomo hayo
yanayohusiana na HIV/AIDS kwa lengo la
kutengeneza vipindi ambavyo vitakuwa na tija kwa jamii kwa kuepuka maambukizi
ya virusi vya ukimwi.
Somo hilo ambalo limewasilishwa lengo likiwa ni kutoa ujumbe
kwa wanachuo hao kuweza kufahamu nini maana ya virusi vya ukimwi pamoja na njia
zinazoweza kuambukiza virusi hivyo ambavyo vimekuwa hatari katika bara la
Afrika.
Hata hivyo mmoja wa anachuo hao bw Ndalike Sonda amesema
wamefurahi kuweza kupatiwa elimu hiyo na wanachuo wenzao ambao ni wakwanza
kutumia mtaala mpya wa masomo na kusema inamfanya kuweza kumjengea uwezo wa kuaandaa
vipindi ambavyo vitaelimisha jamii kuhusiana na maambukizi hayo.
Amesema kuwa waandishi wa habari na mabalozi ambao
wanawelimisha wananchi kwakutumia taaluma hao hivyo kutoa rai kwa kila mwachuo
kueneza elimu aliyo ipata wananchi ili waweze kuelimika.