Shirika la Posta Tanzania lakusanya kiasi cha shilingi Bilioni 44.5 kufikia Mwaka 2012
(Picha na Eliphace Marwa)
Na Frank Mvungi
Shirika
la Posta Tanzania limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi Bilioni
44.5 kufikia mwaka 2012 ikiwa ni matokeo ya kuboreshwa kwa huduma zake
hapa nchini.
Hayo
yamesemwa na Posta Masta Mkuu Bw. Deos Mndeme wakati alizungumza na
waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafaniko
yaliyofikiwa na shirika hilo tangu kuanzishwa kwake.
Mndeme
amesema kuwa mafanikio hayo yametokana na huduma bora zenye hadhi ya
kimataifa zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi hali itakayosaidia
kuongeza mapato ya Serikali.
“Shirika
limejipanga zaidi kutumia TEHAMA katika kuboresha huduma zake ikiwa ni
moja ya mkakati utakaosaidia serikali kuongeza mapato na kufikia malengo
ya muda mrefu yaliyowekwa na shirika pia tumejipanga kuendelea
kuboresha huduma tunazozitoa ili kuendana na mahitaji ya wakati” alisema
Mndeme.
Mndeme
aliongeza kuwa kwa sasa shirika limeunganisha Ofisi 86 kwenye Wilaya na
Miji kote nchini na mfumo wa mawasiliano ili kuongeza idadi ya wateja
wanaohudumiwa,kuondoa ucheleweshaji na kuondoa malalamiko ya wateja.
Katika
kuhakikisha shirika linashiriki kikamilifu katika shughuli za kitaifa
Mndeme alisema shirika litafanya uzinduzi wa toleo jipya la stempu ya
miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe hizo zitakazofanyika
Disemba 28 mwaka huu.
Shirika
la Posta ni mwanachama wa Umoja wa Posta Duniani (UPU) ambalo Tanzania
ilijiunga mwaka 1963 na kwa hivi sasa idadi ya nchi wanachama wa umoja
huo ni 192 malengo ya Umoja huo ni pamoja na kuisimamia,utumiaji wa
barua,Vipeto,Vifurushi katika nchi mbalimbali
duniani,kutoa ushauri,usuluhishi, kuunganisha ushirikiano baina ya nchi wanachama na kutoa misaada ya kiufundi.