RIBERY NDIE MCHEZAJI BORA FRANCE 2013!
ABWAGA POGBA NA MATUIDI!!
KOCHA BORA FRANCE NI RUDI GARCIA!!
Franck
Ribery, ambae ametinga kwenye Listi ya Mwisho ya Wagombea ya Tuzo ya
Mchezaji Bora Duniani, 2013 Ballon d'Or, ametangazwa kuwa ndie Mchezaji
Bora wa France kwa 2013.
Jarida maarufu la Nchi hiyo, France
Football, ambalo ndio walioanzisha Ballon d'Or Mwaka 1956 ili kumpata
Mchezaji Bora Ulaya na kuanzia Mwaka 2010 wakashirikiana na FIFA
kumpata Mchezaji Bora Duniani na kumpa Tuzo iitwayo FIFA Ballon d'Or,
ndio pia hutoa Tuzo ya Mchezaji Bora wa France.
Ribery, anaechezea Klabu Bingwa ya Ulaya
na Germany, Bayern Munich, amewabwaga Kiungo wa Juventus Paul Pogba na
yule wa Paris St Germain, Blaise Matuidi, katika Kura iliyopigwa na
Wachezaji wa zamani na wa sasa wa France.
Hii ni mara ya 3 kwa Ribery kutwaa Tuzo
ya Mchezaji Bora wa France na mwenyewe amesema nia yake ni kuivunja
Rekodi ya Thierry Henry alietwaa Tuzo hiyo mara 5.
Mwaka huu, Ribery aliweza kuisaidia
Klabu yake Bayern Munich kutwaa UEFA CHAMPIONZ LIGI, Bundesliga na
German Cup, na pia yupo kwenye kinyang’anyiro cha Tuzo ya Mchezaji Bora
Duniani, 2013 Ballon d'Or, akichuana na Cristiano Ronaldo na Lionel
Messi na Mshindi wake atatajwa Januari 13.
Nae Kocha wa AS Roma, Rudi Garcia, ambae
alijiunga na Klabu hiyo ya Serie A huko Italy mwanzoni mwa Msimu
akitokea Klabu ya France Lille, na ambe hajafungwa katika Mechi 15 za
Ligi, ndie ametangazwa kuwa ndie Kocha Bora wa France kwa 2013 baada ya
Kura iliyopigwa na Makocha wa sasa na zamani huko France.