CHALENJI CUP: FAINALI KENYA v SUDAN!
MSHINDI WA TATU: KILI STARS v ZAMBIA!!
ZOTE NYAYO STADIUM, NAIROBI, DESEMBA 12!
FAINALI
ya CHALENJI CUP itakuwa kati ya Wenyeji Kenya na Sudan baada ya leo
kuzibwaga Kilimanjaro Stars na Zambia kwenye Nusu Fainali.
Kenya waliifunga Kilimanjaro Stars Bao
1-0 katika Mechi iliyohamishwa toka Machakos na kupelekwa Nyayo Stadium,
Nairobi baada ya Uwanja kufurika maji.
Hata kuko Nyayo Stadium, Mechi hiyo
ilichezwa kwenye mvua na Kenya kufunga Bao lao la ushindi katika Dakika
ya 4 kwa Bao la Clifton Miheso.
Katika Nusu Fainali nyingine, Zambia na
Sudan zilitoka 0-0 katika Dakika 90 na Mechi kuongezwa Dakika 30 ambapo
Sudan walishinda 2-1.
Zambia walitangulia kufunga katika
Dakika ya 110, Mfungaji akiwa Ronald Kampamba na Sudan kusawazisha
Dakika ya 114 kwa Bao la Miaaz Abdelrahim na kupata Bao la usjindi
kwenye Dakika ya 118 lililofungwa na Salah Ibrahim.
Mechi za kusaka Mshindi wa Tatu, kati ya
Kili Stars na Zambia, na Fainali, kati ya Kenya na Sudan, zote
zitachezwa Nyayo Stadium hapo Desemba 12.
VIKOSI:
Kenya:Duncan Ochieng,
Allan Wanga, James Situma, Aboud Omar, Jockins Atudo, Peter Opiyo,
Francis Kahata, Anthony Akumu, Clifton Miheso, David Ochieng Owino,
Edwin Lavatsa.
Akibas: Jerim Onyango, Musa Mohammed,
Paul Muigai Kiongera, Ndetto Mulinge, Noah Wafula, David King'atua,
David Gateri, Jacob Keli
Kili Stars: Ivo Phillip
Mapunda, Kelvin Yondani, Edward Erasto Nyoni, Pius Michael Aidan, Frank
Raymond Domayo, Saleh Dilunga, Ally Samata Mbwana, Alfan Mwrisho Ngasa,
Thomas Ulimwengu, Ramadhan A. Kiemba.
Akiba: Bonevetur Munish, Idd Athuman,
Mao Himid Mkami, Athuman Chanongo, Yahaya Singano Shah Raid Mussa,
Ismail Adan Gambo, Maguli Hassan Mrugau
Refa: Thiery Nkurunziza (Burundi)