CHADEMA YATANGAZA WAGOMBEA WA UDIWANI KANDA YA KASKAZINI
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO – CHADEMA KANDA YA KASKAZINI.(Tanga, Kilimanjaro, Arusha & Manyara)
TAARIFA KWA UMMA
WAGOMBEA WA UDIWANI – KANDA YA KASKAZINI
Tarehe
15 Januari 2014, wagombea wafuatao wa CHADEMA walipitishwa na TUME YA
UCHAGUZI kuwania nafasi za uwakilishi (UDIWANI) katika maeneo ya kata
mbalimbali za kanda ya Kaskazini.
Wagombea
hawa walipita katika mchujo wa uteuzi wa chama. Chama kina matarajio
makubwa sana kuwa wananchi wa maeneo haya ya kata hizi watapata fursa
nzuri ya kuwachagua wagombea wa CHADEMA ambao wana dhamira njema sana na
ya kweli katika kuwatumikia.
Wagombea waliopitishwa pamoja na mikoa yao ni:
JINA LA MGOMBEA
|
KATA
|
JIMBO
|
MKOA
|
BI. MWANAISHA MOHAMED OMARI
|
KIOMONI
|
TANGA DC
|
TANGA
|
BW. KAGOMA FRANK HENRY
|
KIBORLONI
|
MOSHI MJINI
|
KILIMANJARO
|
BW. ALLY BANANGA
|
SOMBETINI
|
ARUSHA MJINI
|
ARUSHA
|
BW. CHARLES SAMWEL MGATA
|
PARTIMBO
|
KITETO
|
MANYARA
|
BW. SANING’O KONE
|
LOLERA
|
KITETO
|
MANYARA
|
Katika
uchaguzi huu CHADEMA imejipanga kushiriki kikamilifu sana tukiwa na
uhakika kuwa chama kimewapa wananchi wapiga kura chaguo lao kwa
kuzingatia uwezo wa wagombea, utayari wa wagombea wetu kushirikiana na
kuwatumikia wananchi na dhamira njema ya kutatua matatizo na kero za
wananchi zilizoletwa na CCM kwa kushindwa kutimiza wajibu wao.
Aidha
chama kimesikitishwa sana na uhuni na ushenzi uliofanywa wa kumteka
mgombea wa CHADEMA ndg. ALLY SAIDI JAHA saa nane mchana siku ya tarehe
15.01.2014 muda mfupi kabla ya muda kurudisha fomu kufungwa. Tukio hili
limetokea huku tukiwa na taarifa zilizopatikana baadae kuwa mida ya saa
nne asubuhi mgombea wetu alifuatwa na kiongozi mmoja wa CCM wa wilaya.
Uongozi
wa kanda tumesharipoti tukio hili polisi na kupewa RB namba
LUS/RB/75/2014 TAARIFA.16.01.2014 ya kutekwa/kupotea kwa ndg ALLY SAIDI
JAHA. Hali kadhalika uongozi chama wa Jimbo la Mlalo umeshwandikia barua
msimamizi wa uchaguzi kuhusu tukio hili la kutekwa nyara na kupotea kwa
mgombea wetu na kuwa baada ya kupata taarifa ya tukio hili kwa kina
chake, chama kitakuwa na mahali pa kuanzia.
Hivi
sasa tumetuma timu ya intellijensia ya chama kuchunguza kwa
kushirikiana na Red Brigade ya wilaya ili kupata undani wa tukio hili
ambalo limetufedhehesha sana na ambalo litakuwa limewanyima demokrasia
ya kuchagua kwa watu wa Mtae ya kiongozi na chama wanachokitaka.
Niwahakikishie
wakazi wa Mtae na Watanzania wote wapenda mabadiliko ambao jambo hili
limetukera wote kuwa ndg Ally Saidi Jaha atatafutwa mpaka apatikane
akiwa mzima au vinginevyo ili ifahamike nini kimemtokea na pia awaeleze
watu wa Mtae na Watanzania wote hili jambo kuna nini nyuma yake. Hapa
kuna mtu au watu watawajibika kwa gharama yoyote, hili jambo halitaisha
kirahisi hivi hivi.
Niwaombe
wakazi wa Kanda ya Kaskazini, kwenye uchaguzi huu tuunganishe nguvu
zetu kwa sisi wenyewe kujitolea na muda wetu na rasilimali zetu, ili
tuwashughulikie CCM ambao wamekuwa wakiendelea kuwatesa Watanzania kwa
sera zao mbovu na uongozi wa kihuni ambao haujali kabisa maisha ya
Watanzania.
Imetolewa na Amani Golugwa
Katibu wa Kanda ya Kaskazini
+255 754 912 914 au 0784 343 275
golugwa@gmail.com