MWENGE WA JUMUIYA YA MADOLA ( QUEENS BATON RELAY) KUTEMBELEA MUHIMBILI JANUARI 19, 2014
Mwenge
wa Jumuiya ya Madola (Queens Baton Relay) utatembelea Hospitali ya
Taifa Muhimbili jumapili ya tarehe 19, Januari, 2014 kuanzia saa tatu
kamili hadi saa nne asubuhi. Mwenge huo unatarajia kufika Hospitali ya
Taifa Muhimbili ukiongozwa na Mheshimiwa Balozi wa Uingereza nchini
Tanzania Bi. Dianna Melrose.
Dhumuni
la Mwenge huo kimataifa ni kutembelea nchi zote ambazo ni wanachama wa
Jumuiya ya Madola katika kuhamasisha maandalizi ya Tamasha la Nne la
Michezo na Utamaduni la Jumuiya ya Madola. Mwenge huu unakimbizwa
kilomita 190,000 kupitia nchi 70 ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya
Madola. Safari ya mwisho ya Mwenge huu itakuwa Julai 23, 2014, Glasgow,
Scotland kwa ajili ya ufunguzi wa sherehe za michezo ya 20 ya Jumuiya ya
Madola.
Hii
ni mara ya tano Mwenge huu kufika nchini Tanzania na utakuwa nchini kwa
siku tatu ukisaidia kuhamasisha ushirikiano, kuimarisha umoja na,
kuongeza ari ya wananchi hususani vijana waweze kuelewa nini maana ya
michezo ya jumuiya ya madola.
Nia
ya mwenge huu kuja Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kutembelea watoto
wanaougua saratani mbalimbali ili kuwapa matumaini ya kuishi na kwamba
jamii inawanathamini. Watoto hawa watapata fursa ya kuushika mwenge huu
na kupiga picha kama kumbukumbu muhimu katika maisha yao.