JIFANU CREATION GROUP IMEITAKA SERIKALI KUIPA KIPAUMBELE SANAA HAPA NCHINI.
Serikali pamoja na mashirika binafsi yametakiwa kuvipa vipaumbele
vikundi mbalimbali vya sanaa hapa nchini kwa kuvisaidia kifedha kwakuwa
vimekuwa ni nyenzo muhimu yakufikisha ujumbe na kuielimisha jamii.
Hayo yamesemwa na viongozi wa Taasisi ya JIFANU ARTS
CREATION katika maeneo ya Unga LTD jiji Arusha walipoongea na Habarijamii
wakieleza namna wanavyofanya shughuli zao katika jamii kwakujitolea na
kufanikiwa kubadili mitazamo ya jamii.
Mkurugenzi mkuu wa Tasisi hiyo Bwana Eliya Masavel amesema sanaa imekuwa na
umuhimu mkubwa sana katika jamii kwa kuwa na mtazamo wenye kuleta tija ndani na
nje ya ngazi za familia na tamaduni mbalimbali.
Amesema licha ya kufanya kazi hizo zikiwemo uhamasishaji wa
Elimu,Utunzaji wa mazingira,Afya pamoja na mambo mengine lakini serikali pamoja
na mashirika binafsi hazina ukaribu na vikundi hivyo jambo ambalo linakwamisha malengo yao kuweza
kutimia.
Kwa upande wa viongozi wengine wa Taasisi hiyo Bw Genesis
Roulen na Bw Ally Juma wamesema kuwa wamefanikiwa kupunguza tatizo la utapia
mlo lililokuwa likiwakabili jamii nyingi,kupinga unanyasaji kwa watoto pamoja
na mambo mengine ikiwa ni moja ya malengo yao.