Header Ads

JUAN MATA: ATAMBULISHWA RASMI.

KUVAA JEZI NAMBA 8!!
JUMANNE USIKU KUANZA RASMI NA ROONEY, ROBIN VAN PERSIE!!
MATA-NA_8MCHEZAJI MPYA wa Mabingwa Manchester United, Juan Mata, Leo ametambulishwa rasmi  na kupewa Jezi Namba 8 huku mwenyewe akisema bado yapo matumaini ya kutetea Ubingwa wao.
Man United wapo Nafasi ya 7 kwenye Ligi wakiwa Pointi 14 nyuma ya Vinara Arsenal huku Mechi zikiwa zimebaki 16.
Mata, ambae amejiunga na Man United hivi Juzi akitokea Chelsea kwa Dau la Pauni Milioni 37.1 ambalo ni Rekodi kwa Man United, huenda akacheza Mechi yake ya kwanza Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford dhidi ya Cardiff City kwenye Ligi Kuu England akivaa Jezi yake Namba 8 ambayo kabla ilikuwa ikivaliwa na Anderson alieenda Fiorentina kwa Mkopo.
Mata, mwenye Miaka 25 na anaechezea Timu ya Taifa ya Mabingwa wa Dunia Spain, amesema: “Ninachopenda kuhusu Klabu hii ni ile imani yao ya kutokata tamaa. Ingekuwa Klabu nyingine iko kwenye hali hii, ingekuwa ngumu kurudi na na kuchukua Nafasi ya Kwanza, lakini Klabu hii inaweza. Huo ndio msimamo thabiti wa Man United, Siku zote wanapigania Mataji, Siku zote wanashinda toka hali ngumu!”
Vile vile, Mata alisema anangojea kwa hamu kucheza na mwenzake Wayne Rooney.
Ameeleza: “Kwangu mimi, yeye ni mmoja wa Wachezaji Bora katika Historia ya Nchi hii. Huwezi kuamini Uchezaji wake. Ni Straika anaeweza kufunga, kusaidia kufunga na kurudi kwenye Kiungo kusaka Mipira. Nitajaribu kushirikiana nae kwa kadri ya uwezo wangu na kusaka mapengo kwenye Difensi za Wapinzani. Nadhani staili yangu nzuri ni kufanya hivyo! ”
Mata, ambae alitokea Valencia ya Spain na kujiunga na Chelsea ambayo aliifungia Mabao 32 katika Mechi zaidi ya 130, ameichezea Timu ya Taifa ya Mabingwa wa Dunia Spain Mechi 32.
Akiongelea ujio wa Mata, Meneja wa Man United David Moyes amesema ameshangazwa kuweza kumsaini Mchezaji Bora kama Juan Mata kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari.
Moyes amesema: “Nimefurahishwa. Tulidokezwa Mwezi mmoja au miwili nyuma lakini sikutegemea kama tutafanikiwa. Tulipopata nafasi kumchukua tuliingia moja kwa moja. Watakuja Wachezaji kama yeye baadae.”
ROBIN VAN PERSIE NA WAYNE ROONEY WARUDI!
Wayne Rooney na Robin van Persie wanaweza kurudi kuichezea Manchester United Jumanne Usiku Uwanjani Old Trafford dhidi ya Cardiff City kwenye Ligi Kuu England.
Rooney amekuwa nje ya Uwanja tangu Januari Mosi Man United walipofungwa na Tottenham alipoumia Nyonga na Van Persie yuko nje tangu Desemba 10 alipoumia Paja kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya Shakhtar Donetsk.
Lakini Mastaa hao wawili wamepona na huenda wakapangwa pamoja na Mchezaji mpya Juan Mata dhidi ya Cardiff City ambayo ipo chini ya Meneja Ole Gunnar Solskjaer, Nguli wa Man United, ambae ni Meneja mpya hapo Cardiff City.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumanne Januari 28
2245 Man Utd v Cardiff
2245 Norwich v Newcastle
2245 Southampton v Arsenal
2245 Swansea v Fulham
2300 Crystal Palace v Hull
2300 Liverpool v Everton
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke
2245 Tottenham v Man City
MSIMAMO:
NA
TIMU
P
GD
PTS
1
Arsenal
22
24
51
2
Man City
22
38
50
3
Chelsea
22
23
49
4
Liverpool
22
25
43
5
Tottenham
22
3
43
6
Everton
22
15
42
7
Man Unit3d
22
9
37
8
Newcastle
22
4
36
9
Southampton
22
4
31
10
Aston Villa
22
-7
24
11
Hull
22
-6
23
12
Norwich
22
-17
23
13
West Brom
22
-5
22
14
Stoke
22
-14
22
15
Swansea
22
-6
21
16
Crystal Palace
22
-17
20
17
Fulham
22
-26
19
18
West Ham
22
-11
18
19
Sunderland
22
-15
18
20
Cardiff
22
-21
18
Powered by Blogger.