PUMA YAIPIGA KIKUMBO NIKE, ‘KUIVISHA’ ARSENAL.
WENGER KUBAKI ARSENAL!
WAKATI
KAMPUNI ya Kijerumani, Puma, ikitangazwa kuwa ndio watakuwa
‘wakiivisha’ Arsenal Jezi kuanzia Msimu ujao kwenye Dili yenye thamini
ya Pauni Milioni 30 kwa Mwaka, Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Iva Gazidis,
amesema Meneja wao, Arsene Wenger, atongeza Mkataba na kubaki nao.
Taarifa hizi za Arsenal kushirikiana na
Puma zinamaanisha sasa Nike, Kampuni ya Kimarekani, ambayo imekuwa na
Arsenal kwa Miongo miwili, imetupwa nje.
Puma, ambao pia ndio wanaivisha Jezi
Borussia Dortmund ya Germany na Timu za Taifa kadhaa ikiwemo Italy, kwa
sasa ni ya Tatu kwa mafanikio katika Kampuini za Jezi na Vifaa vya
Michezo nyuma ya Adidas na Nike.
Nike ndio washiriki wakubwa wa Klabu za Jiji la Manchester, Manchester United na Manchester City na kwa Msimu wa 2012/13 Dili yao na Man United ilikuwa na thamani ya Pauni Milioni 38.
WAKATI HUO HUO, Mtendaji Mkuu wa Arsenal, Iva Gazidis, amesema Meneja wao, Arsene Wenger, atongeza Mkataba na kubaki nao.
Wenger, Miaka 64, ambae yuko Arsenal tangu 1996, amebakiza Miezi 12 ya Mkataba wake wa sasa.
Lakini Gazidis amesema: Arsenal itarefusha Mkataba wakati muafaka na itatangazwa.