MCHUNGAJI MSIGWA ATAKIWA KUELEZA ZILIKO FEDHA ZA VISIMA VYA MAJI ZILIZOTOLEWA NA SABODO
Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Hassan Mtenga katika uzinduzi wa kampeni hiyo |
Baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, Sabodo aliahidi kutoa fedha kwa ajili ya kuchimba visima 200 kwenye majimbo yote yanayoongozwa na chama hicho, alisema Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa, Hassan Mtenga kwenye mkutano huo.
“Muulizeni
Msigwa fedha hizo ziko wapi, mbona jimbo la Iringa Mjini hakuna kisima hata
kimoja kilichochimbwa,” alisema katika mkutano huo ambao Frederick Mwakalebela
alishangiliwa kwa nguvu kubwa na mamia ya wananchi waliohudhuria huku wakimwita
jembe la Uchaguzi Mkuu ujao.
Pamoja
na visima vya Sabodo, Mtenga aliwataka wananchi wa kata ya Nduli na jimbo la
Iringa Mjini kumuuliza mbunge huyo ahadi aliyotoa wakati wa kampeni za Uchaguzi
Mkuu uliopita wa mwaka 2010 ya kuweka wakili ofisini kwake kwa ajili ya kutetea
wananchi masikini imefia wapi.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi alisema tangu Mchungaji Msigwa awe
mbunge wa jimbo hilo miaka mitatu iliyopita, rekodi katika halmshauri yao
zinaonesha amefanya mambo mawili tu kwa wakazi wa jimbo la Iringa Mjini.
Bashir Mtove, mgombea udiwani kata ya Nduli (CCM) akinadiwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Amani Mwamwindi |
Alizitaja
kazi zilizofanywa na mbunge huyo kuwa ni kutoa vitanda 30 vinavyotumia umeme na
baiskeli za miguu miwili 12 katika hospitali ya Manispaa ya Iringa na kugawa
mipira kwa timu za mpira katika kata zote za jimbo la Iringa Mjini.
Alisema
vifaa vilivyotolewa na Mchungaji Msigwa katika hospitali hiyo vilitolewa na
asasi isiyo ya kiserikali ya Reach Out Tanzania for Charity (ROTC).
Viti na vitanda vilivyokabidhiwa na Mchungaji Msigwa katika hospitali hiyo |
Naye
Katibu Mwenezi wa CCM Manispaa ya Iringa, Thobias Kikula alisema katika mkutano
huo kwamba katika moja ya ahadi zake kwa wapiga kura wa jimbo la Iringa Mjini,
Mchungaji Msigwa aliahidi kutenga Sh Milioni 12 kila mwaka kutoka katika
familia yake kwa ajili ya kuchangia shughuli mbalimbali za maendeleo katika
jimbo hilo.
“Muulizeni
tangu kwa miaka mitatu mfululizo amechangia shughuli gani za maendeleo kwa
kutumia fedha hizo,” alisema.
Kikulacho (kulia) |
Mbunge Kigola akinena |
“Muulizeni Mchungaji Msigwa ametembelea nchi ngapi duniani na katika zira zake hizo wakazi wa jimbo la Iringa mjini wamenufaika vipi?” alisema.
Akimnadi
mgombea udiwani wa kata hiyo Bashiri Mtove, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa
aliwataka wakazi wa Nduli kumpigia kura ili amalizie utekelezaji wa Ilani ya
CCM katika kata hiyo.
“Kuna
mradi wa maji wa Sh Milioni 800 katika kata hii; umekuja ikiwa ni utekelezaji
wa Ilani ya CCM, barabara ya Kigonzile inajengwa kwa Sh Milioni 102 na daraja
katika barabara hiyo linajengwa kwa Sh Milioni 54,” alisema.
Alisema
wakati madiwani wa halmshauri ya Manispaa ya Iringa wakipeleka maendeleo kwa
wananchi wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Msigwa anaendelea kupiga kelele
kuhusu tembo na faru.
“Muulizeni
kama jimbo la Iringa Mjini lina hao wanyama?; ni kweli wanyama hao ni
rasilimali ya Taifa na ni muhimu wakalindwa, lakini kuendelea kuwa na mbunge
ambaye hashughuliki na matatizo ya wapiga kura wake na badala yake
anashughulika na mambo ya kitaifa ni hatari kwa maendeleo ya mji wetu,”
alisema.
Alisema
mbali na bungeni, maendeleo ya watu wa jimbo la Iringa Mjini ayanajadiliwa
katika vikao vya baraza la madiwani ambalo yeye sio muhudhuriaji mzuri.
“Amenza
kuhudhuria vikao hivyo mwaka jana, katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo wa
ubunge wake halikuwa haptikani,” alisema.
Mwakalebela naye alipata fursa ya kuzungumza |
Jesca akiwapagaisha wananchi wa kata ya Nduli kwa sera ya amani |
Wengine
waliohutubia mkutano huo ni pamoja na Mwakalebela aliyewasihi wana Nduli
kutofanya makosa kulinda maslai ya kata hiyo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Iringa Jesca Msambatavangu aliyewataka vijana wajiepushe na kampeni za uvunjaji
wa amani zinazofanywa na baadhi ya wanasiasa.