WANAFUNZI WA FANI YA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI ARUSHA WAKAMILISHA RASIMU MPYA YA KATIBA.
Mgeni rasmi ambaye ni mwalimu mlezi wa chuo cha Uandishi wa Habri na Utangazaji Arusha kushoto |
Mgeni Rasmi akikabidhiwa rasimu mpya ya chuo cha A.J.T.C |
Rais wa chuo hicho Bw George Silange akishikana nmkono na katibu wa Rasimu hiyo Bi Emelda Stephano |
Mwenyekiti wa katiba katika Chuo Cha uanadishi wa Habari na Utangazaji Arusha Bw,Oska Samba akimkabidhi mgeni Rasmi rasimu mpya ya katiba. |
Hatimaye wanafunzi katika chuo cha Uandishi wa Habari na
Utangazaji Arusha(A.J.T.C)leo wamekabithi rasimu mpya ya katiba iliyokuwa
ikisubiriwa kwa hamu kwa kipindi kirefu na wanafunzi ili kupata muongozo wa
katiba.
Rasimu hiyo ambayo inapelekea kupatikana kwa katiba mpya imetajwa
kama muhimili mkuu wa uongozi kwa kutoa ufafanuzi na muongozo mkuu wa madaraka
pamoja na mipaka kwa waalimu pamoja na serikali ya wanafunzi na kila mmoja
kupata haki zake za kimsingi.
Akikabidhi rasmi hiyo ya katiba mbele wa mgeni rasimi mwenyekiti
wa tume hiyo Bw,OSKA SAMBA amesema kuwa katiba mpya itato majibu ya kila swali
ambalo wanachuo wamekuwa wakijiuliza na kudai kudai ni hatua kubwa imefikiwa na tume yake kuweza
kukamilisha rasimu hiyo ya awali.
Amesema katika uchambuzi wa rasimu ya katiba hiyo ambayo
itafanyika kuanzia jumanne ya tarehe 28january 2014 utafanyika katika hali ya
amani na upendo na wala sio kwakuwekeana vinyongo kutokana na awali kuonekana
kuleta mvutano na baadhi ya wakufunzi chuoni hapo juu ya utaratibu wa utoaji na
ukusanyaji maoni uliofanyika mwezi mmoja
uliopita.
Pamoja na hayo amesema licha ya kukamilisha rasimu hiyo pia
zipo changamoto ambazo wamekumbana nazo ikiwemo ukosefu wa fedha,baadhi ya
wajumbe kujiuzulu,na kukimbia pamoja na kukatishwa tamaa na baadhi ya watu
wasiopenda maendeleo.
Kwa upande wa mwalimu mlezi wa Chuo hicho cha Uandishi wa
habari na utangazaji Arusha ambaye pia alikuwa mgeni rasmi Bw ANDREA NGOBOLE
Ameipongeza tume ya katiba pamoja na serikali ya wanafunzi kupitia kwa Raisi wa
Chuo hicho Bw George Silange na kusema kuwa wamekuwa wa kwanza kuweza
kuafanikisha rasimu hiyo ikiwa ni moja ya ahadi zao.
Amesema chuo hicho kwa miaka tisa akijawahi kuwa na katiba
ya serikali ya wanafunzi na badala yake ilikuwa ikitumika ya uongozi wa chuo na
kudai na kuwataka wanafunzi hao kuipokea rasimu hiyo kwa furaha na kuhakikisha
katiba mpya inapatikana.