JUMAMOSI MTANANGE WABABE LA LIGA, DIMBANI ESTADIO VICENTE CALDERON!!
UMAMOSI Usiku huko Jijini Madrid, ndani ya Estadio Vicente Calderon, Timu mbili zilizofungana kwa Pointikileleni mwa La Liga, Atletico Madrid na Mabingwa Watetezi Barcelona zitapambana.
Hii ni Mechi inayongojewa kwa hamu sana
hasa baada ya Barca kumkaribisha tena Supastaa wao Lionel Messi aliekuwa
nje ya Uwanja kwa Miezi miwili na Juzi kurejea dimbani kucheza Mechi ya
Copa del Rey na kuifungia Barca Bao 2.
Lakini pia Wadau wanataka kuona Straika
hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa, mwenye asili ya Brazil lakini
ameikana na kuamua kuchezea Spain, nini atakifanya ili kumpiku Cristiano
Ronaldo toka Ufungaji Bora wa La Liga baada Ronaldo kumbwaga kwa Bao 1
hivi Juzi.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
LA LIGA: MSIMAMO Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
FC Barcelona |
18 |
16 |
1 |
1 |
53 |
12 |
41 |
49 |
2 |
Atletico Madrid |
18 |
16 |
1 |
1 |
47 |
11 |
36 |
49 |
3 |
Real Madrid CF |
18 |
14 |
2 |
2 |
52 |
21 |
31 |
44 |
4 |
Athletic Bilbao |
18 |
10 |
3 |
5 |
26 |
23 |
3 |
33 |
5 |
Real Sociedad |
18 |
9 |
5 |
4 |
35 |
23 |
12 |
32 |
6 |
Villarreal CF |
18 |
9 |
4 |
5 |
32 |
20 |
12 |
31 |
7 |
Sevilla FC |
18 |
8 |
5 |
5 |
35 |
29 |
6 |
29 |
8 |
Valencia |
18 |
7 |
2 |
9 |
25 |
29 |
-4 |
23 |
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Barca,
chini ya Kocha Gerardo Martino, wapo kileleni mbele ya Atletico Madrid,
chini ya Diego Simeone, kwa tofauti ya Mabao tu na hivi karibuni
Atletico wamekuwa waking’ara zaidi.
Katika Mechi 5 zilizopita za La Liga, Atletico wameshinda Mechi zote na Diego Costa kupachika Bao 6.
Barca walipata kipigo chao pekee cha La
Liga Msimu huu mwanzoni mwa Desemba walipofungwa 1-0 na Athletic Bilbao
lakini baada ya hapo wakashinda Mechi zao zote 3 na kwenye Mechi hii
wanae tena Messi aliekuwa nje tangu Novemba.
Katika Miaka 20 iliyopita, Atletico na
Barca zimekutana mara 3 tu zikiwa ndio Timu zilizo na Nafasi mbili za
juu kwenye La Liga na Atletico kushinda mara mbili katika Mechi hizo 3.
Msimu huu, wameshakutana mara mbili
mwanzoni mwa Msimu na Barca kutwaa Supercopa de Espana kwa Bao la
Ugenini baada ya kutoka 0-0 Nou Camp na 1-1 huko Estadio Vicente
Calderon.
Kabla ya Mechi hizo za Supercopa de Espana, Barca ilikuwa imeifunga Atletico mara 6.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Uso kwa Uso
[Mechi za karibuni]
-Agosti 28, 2013: Barcelona 0 Atletico Madrid 0 [Supercopa]
-Agosti 21, 2013: Atletico Madrid 1 Barcelona 1 [Supercopa]
-Mei 12, 2013: Atletico Madrid 1 Barcelona 2 [La Liga]
-Des 16, 2012: Barcelona 4 Atletico Madrid 1 [La Liga]
-Feb 26, 2012: Atletico Madrid 1 Barcelona 2 [La Liga]
++++++++++++++++++++++++++++++++++++RATIBA:
Ijumaa Januari 10
2300 Granada CF v Real Valladolid
Jumamosi Januari 11
1800 Athletic de Bilbao v UD Almeria
2000 Celta de Vigo v Valencia
2200 Atletico de Madrid v FC Barcelona
2400 Elche CF v Sevilla FC
Jumapili Januari 12
1400 Getafe CF v Rayo Vallecano
1900 Real Betis v Osasuna
2100 RCD Espanyol v Real Madrid CF
2300 Levante v Malaga CF
Jumatatu Januari 13
2400 Villarreal CF v Real Sociedad
WAFUNGAJI BORA:
1 Cristiano Ronaldo [Real Madrid] Magoli 20
2 Diego Costa [Atletico Madrid] 19
3 Antoine Griezmann [Real Sociedad] 12
4 Alexis Sánchez [Barcelona] 11
Javi Guerra [Real Valladolid] 11
Pedro [Barcelona] 11
7 Ikechukwu Uche [Villarreal] 9
Karim Benzema [Real Madrid] 9
Carlos Bacca [Sevilla FC] 9
10 David Villa [Atletico Madrid] 8
Lionel Messi [Barcelona] 8
Carlos Vela [Real Sociedad] 8
Ivan Rakitic [Sevilla FC] 8
Jonas [Valencia] 8