Header Ads

DEFOE KUHAMIA MLS, AGGER NJE MWEZI, WENGER KUMKOSA MORATA!

>>ROSICKY KUBAKI ARSENAL!
SOMA ZAIDI:
DEFOE KUHAMIA MLS
JERMAINE_DEFOESTRAIKA wa Tottenham na England Jermain Defoe amekubali kujiunga na Klabu ya MLS, Major League Soccer, Toronto FC.
Defoe, mwenye Miaka 31, atajiunga na Klabu hiyo ya Canada inayocheza Ligi ya Marekani, MLS, Februari 28.
Defoe, ambae ameichezea Tottenham Mechi 250, Msimu huu amekuwa hana namba ya kudumu na mara nyingi Meneja alietimuliwa, Andre Villas-Boas, alikuwa akimpiga Benchi na kumchezesha Roberto Soldado na hali hii haikubadilika hata baada ya kuwekwa Meneja mpya Tim Sherwood ambae huwachezesha Emmanuel Adebayor na Soldado.
+++++++++++++++++
TOTTENHAM
WAFUNGAJI BORA:
-Jimmy Greaves - 266
-Bobby Smith - 208
-Martin Chivers 174
-Cliff Jones - 159
-Jermain Defoe - 142
+++++++++++++++++
Defoe amesaini Mkataba wa Miaka minne na Toronto FC lakini yuko huru kuichezea Tottenham hadi Februari 28 na hivyo Mechi yake ya mwisho White Hart Lane inaweza kuwa ile ya EUROPA LIGI dhidi ya Dnipro hapo Februari 27.
Defoe, aliejiunga na Spurs Mwaka 2004 akitokea West Ham, ndie Mfungaji Bora wa Pili kwenye EUROPA LIGI Msimu huu akiwa na Bao 7 ikiwa ni Bao 1 tu nyuma ya Paulo Henrique wa Trabzonspor.
Akiwa na England, Defoe amecheza Mechi 55 na kufunga Bao 19.
BEKI WA LIVERPOOLDANIEL AGGER NJE MWEZI
Sentahafu wa Liverpool Daniel Agger amethibitisha kuwa atakuwa nje ya Uwanja kwa Mwezi mmoja kutokana na maumivu ya Mguu.
Agger, ambae ni Mchezaji wa Kimataifa wa Denmark, aliumia kwenye Dakika za mwisho za Mechi ya FA CUP walipoifunga Oldham Bao 2-0.
Kuumia kwa Agger ni pigo kwa Meneja Brendan Rodgers ambae huenda pia akamkosa Beki Mamadou Sakho anaejiuguza tatizo la Musuli za Pajani.
TOMAS ROSICKY KUBAKI ARSENAL LAKINI MORATA KUTONASWA!
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amethibitisha kubaki kwa Tomas Rosicky hadi mwishoni mwa Msimu lakini pia amepuuza taarifa zilizozagaa za kumchukua Chipukizi wa Real Madrid, Álvaro Morata, kwa Mkopo.
Rosicky, mwenye Miaka 33 na ambae Mkataba wake unamalizika mwishoni mwa Msimu, amesema yeye anataka kubaki Emirates hadi anastaafu lakini hadi sasa si Wenger wala Klabu iliyothibitisha kumwongezea Mkataba.
Huu ni Msimu wa 8 kwa Rosicky kuwa Arsenal lakini Majeruhi ya mara kwa mara yamemfanya acheze Mechi za Ligi 92 tu.
Wakati huo huo, Wenger amepuuza habari zilizozagaa kuwa Arsenal inataka kumchukua kwa Mkopo Chipukizi wa Real Madrid, Álvaro Morata mwenye Umri wa Miaka 21.
Habari hizi zilishika hatamu mara baada ya Juzi kuthibitishwa kuwa Theo Walcott atakuwa nje Msimu wote uliobaki baada ya kuumia vibaya Goti.
Lakini, hapo Jana, mara baada ya Real Madrid kuifunga Bao 2-0 Osasuna kwenye Mechi ya Copa del Rey ambayo Morata aliingizwa mwishoni kutoka Benchi, Meneja wa Real, Carlo Ancelotti, amesema hana nia ya kumwachia Morata kwenda nje kwa Mkopo.
Powered by Blogger.