Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba Akiwasili Katika Ukumbi wa Turbo Mjini Njombe Kuzungumza na Wafanyabiashara. NAIBU WAZIRI WA FEDHA MWIGULU LAMECK NCHEMBA AKIZUNGUMZA NNA WAFANYABIASHARA MJINI NJOMBE LEO MKUU WA WILAYA YA WANGING'OMBE ESTERINA KILASI AKIZUNGUMZA KWA NIABA YA MKUU WA MKOA WA NJOMBE CAPTAIN MSTAAFU ASERI MSANGI AKIWA KATIKA UKUMBI WA TURBO SERIKALI imeendelea kuwasisitizia wafanyabiashara kununua na kuzitumia mshine za mahesabu za kielekroniki za kutolea stakabadhi za EFD wakati ikiendelea kushughulikia hoja zao. Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Lameck Nchemba wakati akiongea na wafanyabiashara wa mkoa wa Njombe na kusema kuwa kitendo cha wafanyabiashara hao kugomea mashine hizo si cha kizalendo na badala yake waombe wapatiwe elimu ili wajue umuhimu wake. Aidha Naibu Waziri Nchemba ameziagiza bodi na mamlaka zinazohusika na masuala ya kusogeza huduma za mamlaka ya mapato Tanzania TRA kuhakikisha wanaanzisha haraka ofisi za TRA Mkoa wa Njombe ili kupunguza gharama kwa wafanyabiashara wanaolazimika kusafiri hadi mjini Iringa ambako kuna ofisi hizo kufuata huduma. Kwa upande wao wafanyabiashara hao wamesema hawapingi kutumia mashine hizo za EFD lakini wakanung’unikia bei zake wakidai zinawauzmiza kwa kuwa ni kubwa zisizolingana na mitaji yao. Baadhi ya wafanyabiashara hao wameiomba serikali kugharamia ununuzi wa mashine hizo huku wengine wakionekana kupinga kuzitumia PICHA ZOTE NA GABRIEL KILAMLYA