NEWS ALERT.AJALI MBAYA YA BASI LA SHABIBY NA PRINCES MUNAA
Abiria 28 wakiwemo watoto wanne wamejeruhiwa baada ya basi
walilokuwa wamesafiria la Kampuni ya Shabiby kugongana na Lori tupu la mafuta
na kupinduka katika kijiji cha Kisaki umbali wa kilometa 10 kwenye Barabara Kuu
ya kutoka Mjini Singida kwenda Dodoma.
Taarifa zilizopatikana kwenye eneo la tukio zimeelezwa kuwa Basi
hilo lenye namba T930BUW aina ya Yutong lililokuwa likiendeshwa
na Dereva wake ambaye
amekimbia mara baada ya ajali hiyo linakadiriwa kuwa na abiria
wapatao 48 lilipata ajali hiyo jana saa 6:50 mchana wakati lilipojaribu
kulipita lori hilo upande wa kulia .
Taarifa hizo ambazo pia zimethibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Singida zinasema kuwa kitendo hicho kilisababisha kuligonga Lori hilo RAA 496N
aina ya MECEDES BENZ lililokuwa likitokea Mjini Kigali nchini Rwanda kwenda Dar
es Salaam likiwa na dereva wake Barimana Benjamini (37) na kuanguka upande wa
kulia wa Barabara na kujeruhi abiria wake .Habari picha kwa hisani ya
superfeoblog.com